Mourinho ametetea hatua ya kikosi chake kucheza soka kwa mfumo wa kuzuia wakati wote, baada ya mashabiki waliofuatilia mchezo huo kusema The Blues walikua wanakera kwa mfumo wa kuzuia muda wote, kwani walitarajia kuona ushindani wa kweli na si upande mmoja kumshambulia mwenzake wakati wote.
Meneja huyo kutoka nchini Ureno, alipata nafasi ya kutoa majibu kwa mashabiki waliokituhumu kikosi chake kwa kusema hawakucheza soka liliowakera bali walicheza vyema huku akiwataka kufahamu kwamba Arsenal ndio wanakera kutokana na kushindwa kutwaa ubingwa wa England, ambapo kwa mara ya mwisho walifanya hivyo msimu wa 2003-04.
Amesema haoni sababu ya kikosi chake kushutumiwa kwa kiasi ambacho anahisi huenda walimuharibia mtu siku yake, zaidi ya kucheza soka kwa namna walivyotaka na kupata matokeo waliyoyahitaji.
Matokeo ya sare ya bila kufungana yaliyopatikana jana katika uwanja wa Emirates, yameipa nafasi Chelsea kuanza kuufikiria ubingwa msimu huu kutokana na tofauti ya point kumi iliopo baina yao na Arsenal sanjari na Man City, huku michezo mitano ikisalia kwa baadhi ya klabu zinazoshiriki ligi ya England.
No comments:
Post a Comment