15 April 2015

DIAMOND NA OMMY DIMPOZI WACHUNIANA BAADA YA KUKUTANA

Screen-Shot-2014-05-19-at-8.14.04-AM 
Kumekuwa na tetesi.. story za mitandaoni ni kwamba msanii Diamond Platnumz hayuko kwenye maelewano mazuri na rafiki yake msanii Ommy Dimpoz, lakini wote wakiulizwa wanakataa kwamba hakuna ukweli wowote.
Soudy Brown akafikishiwa story nyingine kwamba mastaa hao walikutana lakini hawakusalimiana, huku wengine wakisema kwamba Mwasiti amejaribu kuwapatanisha lakini ilishindikana.
Soudy alimtafuta Dimpoz na kumuuliza ishu hiyo, jamaa kasema alikuwa hajui kama Diamond alikuwa eneo hilo na kama angemuona lazima wangeongea… hawana ugomvi wowote kwa hiyo ishu ya Mwasiti kuwapatanisha haipo.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname