01 April 2015

ASKOFU GWAJIMA AMESHINDIKANA,ATOKA HOSPITALI ASEMA HAYA



NA KAROLI VINSENT
        KILE kinachooneka Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima (pichani) ni sawa na sikio la kufa ambalo alisikii dawa,baada ya leo kuibuka na kusema haogopi kulitetea Tamko lilotolewa na jukwaa la kikristo nchini ambalo linawahamasisha waamini wa dini hiyo-
       Kuipigia kura ya Hapana Katiba iliyopendekezwa na Bunge  Maalum la katiba,ambapo amesema atalipinga hata kama serikali ikimwekea vikwazo.
           Kauli kiongozi wa huyo wa Kiroho ameitoa mda huu kwenye Makao Makuu ya Jeshi la polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ambapo alipojisalimisha ili kuhojiwa  mara mwisho baada ya kutoka kwenye Hospitali ya TMJ, Mikocheni Dar es Salaam alupolazwa kutokana kuugua gafla wakati akiwa kwenye mahojiano na Jeshi la polisiwiki iliyopita.
      Akiongea na waandishi wa Habari kwa kujihami mara baada ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi Wilaya kinondoni na kupewa Dhamana na kituoni hapo huku wakijazana waamani wake waliojitokeza na kumpokea Askofu wao.ambapo amesema hawezi kutishika wala kuyumbika kutokana na vikwazo anavyowekewa na Serikali juu ya kuwatetea anaodai wakristo nchini ambao wamewekewa Katiba anayoiita ni mbovu.
         “Mimi nimetoka kwa amani nashukuru sana mungu animeponya salama,ila nasema sitoacha kusema ukweli juu ya wakristo wenzangu ambao anakandamizwa na mifumo ya Katiba ambayo inaonekana wazi”Amesema Askofu Gwajima.
          Askofu Gwajima ameongeza kuwa kwa kuwataka viongozi wenzake kuheshimu tamko la Jukwaa la Kikristo na hata  yeye mwenyewe amesema ataliheshimu sana.
        “Nawaamomba viongozi wa dini wenzangu tuliheshimu Tamko hili la kikristo,na endapo tukiwa tofauti tutakuwa tunakwenda tofauti na tunajivunjia heshima kwa jamii ambapo tulionekana kuwa na msimamo mmoja wakati tukilitoa na mimi mwenyewe nawahakikishia nitalitetea mpaka mwisho”ameongeza Gwajima.
           Alipoulizwa na waandishi wa Habari kuhusu Afya yake amesema hawezi kuzungumzia Afya yake akasema mwenye ruhusa ya kumsemea afya yake, akawataka waandishi kutoendelea kumuuliza huku akiwataka waamini wake kushangilia kwa ushindi waliupata anadai umetokana na nguvu ya mungu.
Kabla ya kulazwa katika Hospitali ya TMJ, Askofu Gwajima alipelekwa katika Hospitali ya Polisi Kurasini na baadaye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo yeye na wafuasi wake waligoma na kutaka atibiwe TMJ ambapo kuna daktari wake maalumu.

Baada ya kujisalimisha kwa mara ya kwanza polisi Machi 27, mwaka huu, Askofu Gwajima anadaiwa kuhojiwa kwa staili ya Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI).
         Inaelezwa alihojiwa na makachero tofauti waliokuwa wakipishana katika chumba cha mahojiano na ambao wanaonekana kubobea katika taaluma hiyo.
Wakati akidhani mahojiano yamemalizika, inadaiwa waliingia maofisa wengine kumhoji maswali tofauti tofauti, mtindo ambao unatumiwa zaidi na wapelelezi wa FBI.
         Hatua hiyo, pia inadaiwa kuchangia kuzimia kwake ambapo awali alidhani mahojiano yangekuwa ni kuhusu kumkashifu Kardinali Pengo tu.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname