Siku ya furaha duniani hii ilikuwa
Ijumaa March 20, huenda ni moja ya sikukuu ambazo hukuwahi kuzisikia
labda, lakini zipo na zinatambulika Kimataifa kabisa.
Pharell Williams ana ngoma yake ya ‘Happy’
ambayo karibu kila mtu anayependa muziki anaipenda na hii pia, ujumbe
wa wimbo huo unahimiza furaha mtu wangu.. lakini ujumbe huo ulimfanya Pharell kuwa
mgeni rasmi kabisa ndani ya ukumbi wa Umoja wa Mataifa na kwenye ujumbe
wake alioutoa alisema kuwa na furaha ni haki yako ya msingi kuipata
tangu unapozaliwa; “happiness is your birthright“– Pharell Williams.
Siku hii ya furaha duniani ilitangazwa rasmi kuanza kuazimishwa mwaka 2012 na Umoja wa Mataifa UN.
Nakusogezea hiki kipisi cha video toka kwenye story ambayo waliiripoti TV ya Al Jazeera.. Pharell akitoa ujumbe wa siku ya furaha duniani.
No comments:
Post a Comment