Tukio moja lilimeibua hisia kubwa kwa wakazi wa kijiji cha
Isyongo kaunti ya nyamira nchini Kenya, baada ya Polisi kufukua
maiti ya msichana mmoja Feidhi Omega 21, iliyokuwa imezikwa chini ya uvungu wa
kitanda.
Taarifa zinasema kuwa binti huyo alimtembelea mpenzi wake
wiki mbili zilizopita lakini hakurudi nyumbani kwao ndipo mama yake alipoanza
kumtafuta na kuelekezwa kwa mpenzi wake Daniel Nyabuti, huku akiwa na matumaini
ya kumkuta mtoto wake akiwa hai,
walipofika nyumbani kwa kijana huyo Polisi walianza kumtafuta na kukuta
kaburi chini ya uvungu wa kitanda kwa kijana huyo ambako binti huyo alikuwa
amezikwa.
“Nikasilia slipaz zimepatikana kwa njia ya huyo kijana baada
ya hapo kufika tarehe karibu tano hivi mwezi wa tatu nikachukua wazee wa
nyumbani kuja hapa tulikuwa watatu tukakuja mpaka nyumbani kwa kijana kuuliza
huyo mtoto” Moraa mama wa marehemu.
Hata hivyo haikuweza kujulikana kilichotokea na kusababisha
kifo cha binti huyo ingawa majirani wamesema walisikia akipiga kelele mtuhumiwa
huyo amekamatwa ili kujua chanzo cha kifo hicho.
Unaweza kutazama taarifa hiyo hapa iliyoripotiwa na kituo
cha K24 kwa kubonyeza play hapa chini…
<<ANGALIA VIDEO>>
No comments:
Post a Comment