Mwanamke mmoja nchini
Nigeria anashikiliwa na Polisi kutokana na kosa la mauaji ya mtu ambaye
alikuwa ni mpenzi wake.. kisa chote kilianzia kwenye ndoto !!
Mwanamke huyo Monsurat
Yusuf alishtuka toka usingizini na kumsimulia mpenzi wake,Eric Moses
kwamba ameota ndoto ambayo alihisi amepigwa na mpenzi wake huyo makofi
akiwa usingizini.
Eric alicheka baada ya
kusikia story hiyo lakini kumbe Monsurat hakupenda, akachukua kisu na
kumchoma mpenzi wake huyo ambaye alifariki.
Upelelezi wa Polisi umeonesha wote wawili walikuwa ni wanafunzi na walikuwa wakiimba kwaya pia ya kanisa.
No comments:
Post a Comment