Mshambuliaji
wa Emmanuel Emenike wa Fenerbahce amekuta akishindwa kujizuia na
kulazimisha afanyiwe mabadiliko na kutolewa nje hata kabla ya kipindi
cha pili.Katika
mechi hiyo ya Ligi kuu ya Uturuki dhidi ya wapinzani wao Besiktas,
Emenike raia wa Nigeria alilazimisha kutoka na kuvua jezi wakati
mashabiki walipoanza kumshambulia kwa maneno makali yakiwemo ya
kibaguzi.
Mashabiki hao walikuwa wakimzoea baada ya kushindwa kutuliza mpira mrefu aliopigiwa.
Hali hiyo ilionyesha kumuudhi ingawa mashabiki hao pia walilalama kwamba msimu huu amekuwa hana msaada kwa timu yao.
Pamoja
na kufanikiwa kutoka, Emenike alirudishwa na benchi la ufundi akiwemo
kocha wa timu hiyo ambaye hata hivyo baadaye alilazimika kumtoa baada ya
kipindi cha kwanza kwisha.
Ubaguzi
wa rangi umekuwa ukiendelea katika nchi mbalimbali ikiwemo Uturuki
ambayo ndiyo nchini pekee duniani iliyo katika mabara mawili ya Asia na
Ulaya.
Asilimia
kubwa ya Waturuki ni wale wenye asili ya Waarabu, lakini ajabu nao
wamekuwa na tabia hizo mbovu za kishenzi za ubaguzi wa rangi.
No comments:
Post a Comment