03 March 2015

Haya ndiyo majibu ya mwimbaji Rama Dee kuhusiana na muziki wa Kinigeria kuteka soko na masikio ya watu wa Tanzania



Wasanii wengi wamekuwa wakizungumzia kuhusiana na suala hili la muziki wa Kinigeria kuteka soko na masikio ya watu wa Tanzania, Juzi alikuwa ni msanii Ben Pol lakini pia katika ku peruzi nikakuta kuwa Rama Dee naye kwenye ukurasa wake wa facebook aliamua kuongelea suala hili pia.

Kupitia ukurasa wake wa facebook aliandika haya kuhusiana na muziki wa Kinigeria kuteka soko na masikio ya watu wa Tanzania.
Nigria ni Nchi kubwa sana kuliko kwetu pia muziki wao sio mbaya ni mzuri na kikubwa zaidi jamaa wanaunyumbani yani kusaidiana "UZALENDO" so kwa sisi tunachotakiwa kufanya ni kupiga kazi nzuri zaidi na kuwapa Watu nafasi zaidi ya kutoboa.... Nigeria ipo ndani ya Africa na jamaa wakitoka nje ya Africa wanatuwakilisha mpaka sisi Watanzania......mimi nikiona Mtu analalamikia wanaigeria naona kama amewashindwa hawa jamaa wala sio wazito kutokana na sound yetu ya kibongo chamsingi tupige kazi tu tuache kuongea....... Tupige mangoma makali tutupie kwenye nchi yao wapambane nayo...... Wewe ngoma kama KUWA NA SUBIRA davido anaweza kuiimba na ile sauti ya konyagi kweli ?????hebu tupigeni kazi bwana!!!!"

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname