UMOJA WA VIJANA CCM (UVCCM)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
AMBASADA LU
YOUQING NA MHE .MASELE WAZUNGUMZA JUU YA MKUTANO WA JUKWAA LA VIONGOZI VIJANA AFRIKA NA
CHINA
20/ Machi/
2015, Dar es salaam, Balozi wa China nchini Tanzania Dr. Lu
Youqing na Naibu waziri Ofisi ya makamu wa rais (Mazingira) Mhe. Stephen Masele
wamekutana leo kuzungumzia mkutano wa
kimataifa wa viongozi vijana wa Afrika na China unatorajiwa kufanyika kuanzia Machi 27 na kumalizika Machi 31 katika
Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto, mkoani Arusha.
Jukwaa hilo la
viongozi vijana lenye lengo la kuhamasisha ushirikiano na kujenga uhusiano mwema
kwa ajili ya kukuza uchumi, linatarahiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, ambapo atahutubia wageni
waalikwa kutoka zaidi ya nchi 40, huku mambo mbalimbali yakiwasilishwa kwa
ajili ya kujadiliwa kwenye jukwaa hilo.
Akiongea na
waandishi wa habari katika Ubalozi wa watu wa china hapa nchini, Dr. Lu Youqing
alitoa maoni yake juu ya mkutano huo sambamba na kutaja baadhi ya maeneo ambayo
viongozi vijana wa China wangependa kujifunza wakati wa mkutano huo.
“Tunafahamu kwamba China ni mwekezaji mkubwa
sana kwenye nchi za Afrika na kila siku tuona biashara za aina mbalimbali
zinazofanyika baina ya bara la Afrika na nchi ya China. Tanzania ni nchi
mojawapo Afrika ambayo China imewekeza zaidi na kupitia mkutano huu ninaamini
kuwa urafiki wetu pamoja na uchumi kati yetu utaendelea kukua zaidi”
Tofauti na urafiki mzuri ulio baina ya nchi hizi mbili Balozi Lu Youqing
aliongeza kuwa uchumi wa Tanzania unaridhisha na unaendelea kukua kila siku,
huku akitaja kuwa ndio sababu kuu ya kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa
mkutano huu wa kimataifa.
Kwa upande wake Naibu waziri wa nchi Ofisi ya makamu wa Rais
(Mazingira) Mhe. Stephen Masele ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa kamati ya
maandalizi ya mkutano huo alisema…“Dhumuni
kubwa la mkutano huu ni kuimarisha uhusiano mzuri ulipo kati ya China na Afrika
lakini pia ni fursa muhimu kwa vijana wafanyabiashara kupanua mawazo yao na
kufungua milango ya kibiashara kati ya Afrika na China”. Mhe. Masele
alitaja baadhi ya maeneo yatakayopewa kipaumbele ni kama Fedha na uwekezaji,
Kilimo, Madini, Uchumi na Biashara.
“Tunatarajia ugeni wa zaidi
ya vijana 200, Afrika ina vijana wengi ambao tunaamini kupitia mkutano huu
wataweza kujifunza fursa mbalimbali za kujenga maisha yao ya baadae iwe ni
kiuchumi au siasa” …aliongeza Masele.
Alimalizia kwa kukishukuru chama cha mapinduzi kwa kuonyesha
ushirikiano thabiti wakati wa kipindi hiki amabacho wapo kwenye mchakato wa
maandalizi ya mkutano huo.
No comments:
Post a Comment