Jumanne 03/02/2015: I&M Bank (T) Limited imeendelea
kuonyesha muelekeo mzuri katika soko baada ya kuzindua huduma ya kwanza na ya
kipekee ya ya kibenki ijulikanayo kama “Banking
lounge” itakayokuwa ikifanya kazi kwa masaa 24 kwa siku saba, ndani ya ghorofa
ya kwanza katika jengo la Viva Towers, moja kati ya maeneo muhimu jijini Dar es
salaam. Tanzania.
Hili ni
jaribio la kipekee kwa Benki hiyo, kutoa huduma mbalimbali za kibenki kama
vile;-Mashine ya kubadilisha fedha za kigeni, mashine ya mfumo wa ATM ya kuweka
na kutoa fedha, “Siku yoyote, muda wowote” ndani ya masaa 24 katika siku saba
za wiki.
MASHINE YA KUBADILISHA FEDHA ZA
KIGENI: Ni sehemu ya
kubadilishia fedha itakayokuwa ikifanya kazi kwa muda wa masaa 24 ndani ya siku
saba za wiki. Hii itamuwezesha mteja kubadilisha fedha zake za kigeni na
kupokea shilingi ya kitanzania bila ya kuwa na mtoa huduma. Hii itakuwa na
umuhimu zaidi kwa wateja ambao watapenda kufanya miamala yao hasa nyakati za
jioni/usiku huku kukiwa hakuna haja ya mteja kuwa na akaunti ya benki hiyo pindi
anapotaka kupata huduma hii bali anachohitaji ni pasipoti halali ili kupata
huduma.
MASHINE YA KUWEKEA FEDHA: Itamsaidia mteja kupata huduma kwa
masaa 24 ndani ya siku saba hasa kwa maduka na biashara yanayofungwa mida ya
jioni/usikuili kuweka fedha za mauzo yao ya siku nzima katika akaunti za benki
zao muda wowote. Huduma hii ni ya kila siku ikiwemo siku ya jumapili na siku za
sikukuu. Benki hii imefunga “kifaa maalum cha kuwekea fedha”, ambacho kiasi chochote
kikubwa cha fedha kinaweza wekwa kwa usalama wa hali ya juu katika mashine hiyo
pasipo na uhitaji wa mtoa huduma wa benki.
Mashine
hii itahesabu fedha na itatoa risiti kwa mteja. Mashine hii ina kasi ya ajabu
na uwezo mkubwa wa kuweka fedha nyingi, ikiwa na teknolojia ya hali ya juu kama
vile kitambua fedha endapo itakua ni feki au la, kichambuzi na kitambuzi namba n.k.
MASHINE ZA ATM: Mashine za ATM zilizowezeshwa na
VISA zitakazokuwa zikifanya kazi kwa masaa 24 zitawahudumia wateja na wa
watumiaji wa kadi za VISA.
Zaidi
ya huduma hizi za hali ya juu, Benki pia imeanzaisha “VIP SERVICE LOUNGE” ambayo inatoa huduma ya kibenki isiyo ya fedha,
katika hali ya kisasa na starehe. Ikiwa na TV na mashine za kujipatia kahawa, mteja
anaweza kukaa na kupumzika, katika hali salama, wakati wahudumu waliofunzwa kwa
umahiri wakiendelea kumhudumia, kuanzaia saa 2 asubuhi mpaka saa 2 usiku. Pia wahudumu
watasikiliza na kupokea mahitaji yote ya wateja yatakayotolewa huduma katika
tawi letu la Maktaba kama vile:-maombi ya kufunguliwa akaunti, maombi ya
TT/TISS, huduma za vitabu vya hundi, kadi za malipo ya kabla ya fedha za kigeni,
huduma ya kadi za ATM, mikopo, maombi ya kadi za BPesa, taarifa nyingine za
kibenki na msaada katika huduma nyingine za kibenki.
I&M
imekuwa ni benki ya kwanza kuanzisha huduma hii ya teknolojia ya hali ya juu
katika soko la Tanzania ambapo “Smart Banking Solutions Ltd” kwa mara nyingine
tena imepiga hatua kwa kuungana na benki hiyo na kufunga mashine za kuweka na kutoa fedha sambamba na
kubadilishia fedha za kigeni.” .
Akielezea
faida za mfumo huu, Afisa mtendaji mkuu wa benki ya I&M
Bw. Anurag Dureha alisema “Kwa mfumo huu mpya mteja wa I&M sasa
atakuwa na uwezo wa kutumia huduma za kibenki kwa urahisi”. Tawi hili jipya linampa
mteja njia mbadala za kufanya miamala, zaidi ya ile ya awali kama vile matawi
ya benki, intaneti na simu za mikononi.
“Kwa
kuanza, fedha ya kigeni itakayobadilishwa na mashine hizi ni dola za kimarekani
muda mfupi baadae tutaongeza fedha nyingine za kigeni ili kutimiza mahitaji ya
wateja wetu wanaotoka sehemu mbalimbali duniani kote” aliongeza Bw. Dureha
No comments:
Post a Comment