Baadhi
ya watumiaji wa mtandao wa Facebook wameanzisha kampeni kubwa kuitaka
kampuni hiyo kuondoa picha za binti mdogo mwindaji anayeonekana amepiga
picha na wanyama wakali anaodai kuwaua katika nchi za kiafrika ikiwemo
Zimbabwe.
Binti
huyo Kendall Jones kutoka Cleburne, Texas, anadaiwa kuwa ni mwindaji
mdogo zaidi kuwapiga risasi wanyama hao wakali wa mwituni akiwemo Chui
na kuthibitisha hilo amekuwa akipozi nao kwa picha baada ya kufanya
kitendo hicho.
Maelfu ya watu wanaitaka Facebook kuondoa picha hizo ambapo binti huyo amejitetea kuwa anafurahi kuendeleza ndoto zake.
Binti
huyo amekuwa akitabasamu na kuweka pozi pembeni ya wanyama wa aina
mbalimbali anaodai kuwaua ambapo picha hizo zimeamsha hisia kali katika
mitandao ya kijamii watu wakidai ziondolewa.
Mmoja
wa mashabiki amenukuliwa akisema kuwa”Kwa vyovyote vile
utakavyoangalia, kuona mtu anatabasamu pembeni ya mwili uliokufa ni
kitendo cha kuhuzunisha sana.”
No comments:
Post a Comment