Staa huyo ameshinda kipengele cha wimbo bora wa Afrika Mashariki, ‘East Africa Super Hit’ kwa wimbo wake ‘Number One.’
Diamond alikuwa akichuana na nguli wengine wa muziki kutoka Kenya, Uganda na Rwanda.
“Thank you so much Uganda / Hipipo Awards for this Awards, it means alot to me.. i will always make sure that i work hard and give my East and Africa proud…..S/O to my boy Tom Lee, and all team @wcb_wasafi #East_Africa_Super_Hit #JusWokeuplikeDat,” ameandika Diamond.
Hizi ndio nyimbo zilizokuwa zikiwania kipengele cha wimbo bora wa Afrika Mashariki:
- Tayali – Urban Boys Ft Iyanya
- Sitya Loss – Eddy Kenzo
- Ndagushima – Ommy Dimpoz
- Number One – Diamond Platnumz
- Nishike (Touch Me) – Sauti Sol
- Love You Everyday – Bebe Cool
- Kioo – Jaguar
- Baramushaka – Knowless
Katika tuzo hizo, Bebe Cool ndiye aliyeibuka na tuzo nyingi zaidi ikiwemo ya msanii bora wa mwaka. Muimbaji huyo ameshinda tuzo sita.
No comments:
Post a Comment