Jeshi la wananchi kwa kushirikiana na polisi nchini limeongeza askari
wa vikosi vya ardhini katika zoezi la kukabiliana na vikundi
vinavyodaiwa kuwa vya kigaidi katika mapango ya mleni yaliyopo eneo la
amboni jijini Tanga kufuatia askari wa jeshi la wananchi kuuawa kwa
risasi huku wengine wakijeruhiwa katika mapigano baina yao na vikundi
hivyo.
Hata hivyo baadhi ya familia zilizopo katika eneo la Mleni
zinadaiwa kuhamisha makazi kufuatia milipuko ya risasi na silaha nzito
za kijeshi zilizokuwa zikirindima katika kipindi cha siku mbili nyakati
za mchana na usiku, hatua ambayo baadhi ya makundi ya vijana
yanaojihusisha na kazi ya kupasua mawe katika mapango hayo kulalamikia
ukosefu wa kazi kwa sababu ya mapigano hayo ambayo pia yamewapa hofu na
maisha yao
ITV imeshuhudia msafara wa magari ya kijeshi pamoja na yale ya
maofisa wa kijeshi na huduma ya kwanza yakipita katika barabara kuu
itokayo Tanga kwenda Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania kisha
kuingia katika njia iendayo katika mapango yaliyodaiwa kuwa ni sehemu
maalum ya maficho ya vikundi hivyo vya kigaidi na msemaji wa polisi
kamishna wa polisi -operesheni Paul Chagonja kutwa nzima simu yake
iliita bila majibu lakini msaidizi wake alipoke na kudai kuwa bosi wake
yupo kwenye kikao.
No comments:
Post a Comment