Baraza
la Taifa la Elimu ya Ufundi ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya
Bunge Namba 9 ya Mwaka 1997, kwa lengo la kusimamia na kuratibu taaluma
zitolewazo na taasisi na vyuo vya elimu ya ufundi nchini, ambavyo siyo
vyuo vikuu au vyuo vikuu vishiriki. Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza
na kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini kwa kusimamia
kikamilifu shughuli za uendeshaji mafunzo ili tuzo zitolewazo na vyuo
ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa.
Notisi
Notisi
Kwa
kutumia Sheria na Kanuni za Baraza [National Council for Technical
Education (Registration of Technical Institutions) Regulations, 2001 na
National Council for Technical Education (Accreditation and Recognition
of Technical Institutions) Regulations, 2001 Baraza linatangaza kwamba
linatoa notisi ya siku 30 kwa vyuo/taasisi ziilizokiuka taratibu za
Usajili na Ithibati zifuatazo:
a) Vyuo/Taasisi ambazo muda wake wa Usajili wa Awali na Usajili wa Muda umekwisha;
b) Vyuo/Taasisi ambazo zimepitisha muda wa kuanza mchakato wa Ithibati baada ya kupata Usajili Kamili; na
c) Vyuo/Taasisi ambazo muda wake wa Ithibati umekwisha.
Vyuo/taasisi ambazo zinapewa notisi ni kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali Na. 1 na Na. 2.

No comments:
Post a Comment