04 February 2015

MASKINI ISABELA WA LUTENI KARAMA: MIMBA NNE ZAHARIBIKA!


Laurent Samatta/Uwazi 
BAADA ya kuachana rasmi mwanzoni mwa mwaka huu, Isabela Mpanda ‘Bela’ na Luteni Karama,msanii huyo wa kike ameamua kumwaga mchele kwa kudai kuwa aliwahi kushika mimba zaidi ya nne za Karama na zote zikaharibika.
Msanii wa filamu Bongo,Isabela Mpanda ‘Bela’.Akifunguka mbele ya paparazi wetu, Bela alisema alikuwa akishika mimba hizo lakini zote zilikuwa zikiharibika baada ya kufikisha miezi minne tu. 
“Nilikuwa napenda kumzalia Karama lakini kila alipokuwa akinipa mimba zote zilikuwa zikiharibika, ameshanipa mimba nne na zote zikawa hivyohivyo. Sijui lakini labda damu zetu zilikuwa haziendani kwenye mimba,” alisema Bela.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname