Rapa anayechipukia Rymir Satterthwaite
anasema Jay z ni baba yake mzazi na anataka vipimo vya DNA. Kijana huyu
mwenye miaka 21 anasema Jay Z alikuwa na mahusioano na mama yake kwenye
miaka ya tisini na kwamba walikuwa pamoja kwa muda mrefu kabla hajawa
maarufu.
Rymir anataka vipimo vya DNA Ila Jay z
hajakubali kufanya hivyo ndio maana mpaka sasa kijana huyu amechukua
hatua ya kwenda mahakamani kutaka mahakama ilazimesha vipimo hivyo.
Rymir analalamika kuwa ameishi kwenye maisha ya shida huku baba yake
akiwa tajiri kwa muda mrefu. Jay Z anajulikana kuwa na mtoto mmoja tu
ambaye ni Blue Ivy Carter na mke wake ambaye ni Beyoncé Knowles
No comments:
Post a Comment