STAA mkongwe katika tasnia ya filamu, Blandina
Chagula Johari amefunguka kuwa kamwe hatarajii kuolewa na staa kama
Vicent Kigosi Ray bali anahitaji mume wa kawaida asiye maarufu.
Akizungumza na Uwazi, Johari alisema kuwa kwa upande wake hachagui
mwanaume gani wa kumuoa bali tu ajue kumthamini na kumuheshimu kama
mwanamke.
Staa mkongwe katika tasnia ya filamu, Blandina Chagula Johari.
Kwanza sihitaji mwanaume wa kunioa awe staa hata siku moja, nataka tu
awe wa kunijali na kunithamini na kingine awe mchapakazi kwa kuwa mimi
mwenyewe ni mtafutaji, alisema Johari.
Awali, Johari aliwahi kuripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na
nyota wa filamu, Ray na kuachana baadaye. Kama ni hivyo basi mapenzi yao
yalikuwa ni ya boyfriend na girlfriend na wala si ndoa
No comments:
Post a Comment