17 February 2015

JEURI YA PESA HILI NDO GARI JIPYA LA MSANII AY--AINA YA RANGE ROVER SPORT---DAZ BABA APAGAWA BAADA YA KULIONA


Msanii wa zamani wa kundi la Daz Nundaz, Daz Baba amemmwagia sifa kibao rapper Ambwene Yessayah aka AY kuwa ni msanii wa kuigwa.
Daz Baba akiwa katika makaburi ya Kisutu kwenye mazishi ya baba yake Dully, Ebby Sykes

AY alitinga kwenye mazishi ya Mzee Ebby Sykes akiwa kwenye Range Rover ya rangi ya kijivu kitu ambacho kilimvutia Daz Baba.

Daz ameiambia Bongo5 kuwa AY ni mshikaji wake toka kipindi cha nyuma na anavutiwa na hustle zake.


AY akiondoka katika makaburi ya Kisutu baada ya mazishi ya Ebby Sykes akiwa kwenye Range Rover

“AY yuko vizuri sana, ni mfano wa kuigwa, mzee wa commercial toka kitambo anafanya muziki mzuri ndo maana unamuona hivyo, ” alisema Daz. “Jamaa anajituma, anafanya kazi kwa bidii ndio maana unaona hayo mafanikio yote,” aliongeza.

Pia Daz amesema kuna mpango wa kufanya ngoma na muimbaji huyo wa ‘Zigo’.

“Nina mpango wa kufanya naye kazi. AY ni mshkaji wangu toka kitambo kwahiyo kila kitu kitaenda sawa.”

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname