Mwaka jana mwishoni (2014) baada ya Diamond kukutana na wasanii
wakubwa wa Afrika wakiwemo Fally Ipupa na P-Square nchini Nigeria,
alisema “nikikutana na 18 huwa naachia bonge la shuti mpaka nishinde” na
kauli yake imetimia.
Staa huyo wa ‘Ntampata Wapi’ amefanikiwa kufanya collabo na staa wa DRC,
Fally Ipupa ambayo ni miongoni mwa nyimbo nne alizopanga kuzitoa kati
ya sasa na mwezi wa tatu.
Meneja wa Diamond, Babu Tale amesema kuwa wanampango wa kutoa nyimbo nne
mfululizo hadi kufika mwezi wa tatu 2015, zikiwemo za Diamond na
zingine alizofanya collabo na wasanii wa nje.
“Huu mwaka tunaugeuza vizuri kutoka January mpaka March tuna release
nyimbo nne mfululizo ambazo ni za Diamond na zingine ni za watu wa nje
ambao feauturing Diamond. Fally ametokea kumkubali Diamond, kwahiyo
ngoma inakuwa ya Fally na Diamond, kila mmoja anafanya kwenye sebule
yake tunakutana kwenye video kama ni Godfather, kama ni Adam, kama ni
Moe Musa kama ni nani yeyote yule” Alisema Babu Tale kupitia Amplifaya ya Clouds Fm.

No comments:
Post a Comment