Polisi nchinikenya katiika mji mkuu Nairobi leo imewafyetulia gesi ya
kutoa machozi wanafunzi wa shule ya msingi waliokuwa wakiandamana
kupinga unyakuzi wa ardhi waliyokuwa wanatumia kama kiwanja cha kuchezea
na mmiliki binafsi.
Polisi hao wakiwana Mbwa waliwatawanyta wanafunzi hao, baadhi yao
wakisemekana kuwa watoto wenye umri wa miaka sita baada ya kuuangusha
ukuta mpya uliojengwa kati ya shule yao na uwanja huo.
Wanafunzi hao walikuwa wamerejea shuleni Lang'ata baada ya mgomo wa wiki
mbili wa walimu wa shule za umma walipopata kiwanja chao kikiwa
kimeuzwa na hata kuwekwa uzio.
Shule hio ina karibu watoto 1,000 walo kati ya umri wa miaka mitatu na kumi na minne na inasimamiwa na baraza la jiji.
Baraza la jiji limesema kuwa ardhi hio ni ardhi ya serikali ingawa
halijazungumzia ambavyo ardhi yenyewe iliuzwa ingawa wanaharakati
wanasema kiwanja hicho kimeuzwa kwa tajiri anayepanga kukitumia kwa
ujenzi
No comments:
Post a Comment