SIMBA haina mwenendo mzuri katika Ligi Kuu Bara lakini kuna neema kidogo
kwa wachezaji wake; beki wa kati Hassan Isihaka na straika Ramadhan
Singano aliyewahi kupachikwa jina la Messi.
Neema yenyewe imekuja baada ya klabu ya Real Madrid ya Hispania kuomba
CD tano za picha zao za video wakiichezea Simba katika mechi za hivi
karibuni.
Maofisa wa Real Madrid ambao wapo nchini, wameuomba uongozi wa Simba
uwapatie CD hizo za wachezaji hao ili watazamwe vizuri kabla ya kuwapa
nafasi ya kufanya majaribio katika timu yao ya vijana.
Bosi mmoja wa Simba aliliambia Mwanaspoti akisema: “Real Madrid
wametuomba hizo CD za Isihaka na Messi ili wazione na wakiridhika zaidi
watawachukua kwa majaribio katika timu zao za vijana.”
Maofisa hao wa Madrid ambao wapo nchini kuanzisha mradi wa kituo cha
kukuza soka la vijana, waliona uwezo wa Isihaka na Messi katika mchezo
wao dhidi ya Azam FC wikiendi iliyopita ambao ulimalizika kwa sare ya
bao 1-1.
No comments:
Post a Comment