‘Diamond Platnumz’ akifurahia jambo na Peter Okoye wa 'P Square'.
Stori: Musa Mateja
MWACHENI Diamond
aitwe Diamond! Hiyo kauli pekee unayoweza kuisema kufuatia wakali wa
muziki wa R&B kutoka Nigeria, Peter na Paul Okoye ‘P-Square’
kuukubali uwezo wa kimuziki wa bwa’mdogo kutoka Tandale, Bongo, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ijuma Wikienda linakupa mchapo hatua kwa
hatua.
Bwa’mdogo kutoka Tandale, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa madansa wake ndani ya Lagos, Nigeria.
NI LAGOS, NIGERIA
Wakali
hao walionesha kumpigia saluti Diamond baada ya kukutana naye kwenye
tamasha la utoaji wa Tuzo za Wanamichezo Bora Afrika lililofanyika
Lagos, Nigeria, usiku wa kuamkia Januari 9, mwaka huu.
WALIANZIA HOTELINI
Kwa
mujibu wa chanzo kilichoambatana na Diamond nchini humo, saa chache
kabla ya shoo kuanza, P-Square walimuibukia kwenye Hoteli ya Eko
aliyofikia jijini humo na kummwagia pongezi nyingi sambamba na kumshauri
baadhi ya vitu vya kimaendeleo.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo
hicho kilisema, P-Square walionekana kuvutiwa zaidi na juhudi binafsi
za Diamond kiasi cha kuweza kuipeperusha bendera ya Afrika Mashariki
katika levo za kimataifa.
“Jamaa
walipomuona tu hotelini waliguswa sana na juhudi zake binafsi maana
wanatambua jinsi gani muziki ulivyokuwa mgumu kuuvusha nje ya nchi yako
lakini kwa kuwa Diamond ameweza, walimpigia saluti,” kilisema chanzo
hicho.
ARUHUSIWA KOLABO
Chanzo
hicho kilizidi kumwaga data za ndani kwa kusema, mbali na kumpigia
saluti, P-Square walionesha wako tayari kumsapoti Diamond kwa kumpa
nafasi ya kufanya nao kazi yaani kolabo.
“Wamempa
nafasi ya kufanya naye kazi pale atakapojisikia kutokana na mipango
yake, kama akiamua kufanya sasa au baadaye ni uamuzi wake lakini jamaa
(P-Square) hawana kinyongo naye lengo lao ni kuona muziki wa Afrika
unateka dunia,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
‘Diamond Platnumz’ akiwa na Paul Okoye wa 'P Square'.
“Walimwambia
the way (namna) alivyo na juhudi kwenye kazi yake anatambulika Nigeria
utafikiri ni msanii kutoka Nigeria, walimpa mbinu zao za namna
walivyopigana hadi kufika hapo walipo.”
No comments:
Post a Comment