Mwigizaji wa filamu Bongo, Rose Ndauka.Na Laurent Samatta
KAMA kawa kama dawa, tunakutana tena katika safu yetu ya Sindano 5, kutokana na maombi mliyonitumia wiki iliyopita tulipoianza safu hii, leo tunawaletea mwigizaji Rose Ndauka ambaye wengi mlimpendekeza awepo katika safu hii.
Mahojiano kati yake na paparazi wetu yalikuwa hivi:
•Paparazi: Rose Ndauka mambo vipi? Siri ya urembo wako ni nini maana kuna tetesi kwamba mkorogo ndiyo unaokufanya uonekane mzuri?
Rose Ndauka: Siri ya urembo wangu anaijua Mungu. Hakuna zaidi ya hapo. •Paparazi: Umeachana na mzazi mwenzio, Malick Bandawe ambaye mliishi kwa muda mrefu, nini unakimisi kutoka kwake.
Rose Ndauka: Hakuna ninachokimisi kutoka kwake. Maisha yanaendelea!
•Paparazi: Unakumbuka kiasi cha fedha ulichoanza kulipwa katika kazi yako ya kwanza?
Rose Ndauka: Ndiyo nakumbuka, muvi ya kwanza nililipwa laki tatu tu.
Rose Ndauka akiwa na mzazi mwenzake, Malick Bandawe. •Paparazi: Msanii gani wa kiume unayemkubali sana Bongo Movies?
Rose Ndauka: Kiukweli namkubali sana Single Mtambalike ‘Richie Richie’.
•Paparazi: Wasanii wengi wanapoanza maisha huwa wanapangiwa chumba na wanaume, wewe ulipoanza ulipangiwa na nani?
Rose Ndauka: Sikupangiwa na mwanaume yeyote, nakumbuka kwa mara ya kwanza wakati naanza kupanga nililipa laki moja na ishirini mwenyewe!
Unapenda msanii gani atokee kwenye safu hii? Comment jina lake hapo chini tafadhali!
No comments:
Post a Comment