UCHUMI SUPERMARKETS LTD
TANZANIA
![](file:///C:\Users\Jambo\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image002.jpg)
RE: MKAZI WA KINONDONI AWA MMLIKI MPYA WA UCHUMI
SUPERMARKETS TANZANIA
Maduka makubwa yanayoongoza Tanzania ya “Uchumi
supermarks” leo yameendesha droo ya mwisho ya kampeni yao ijulikanayo kama “Mimi Mwanahisa promosheni” iliyofanyika katika
tawi lake jipya la Mbezi-Kawe.
Hafla hiyo ilishuhudiwa na Mheshimiwa Said Meck
Sadik- Mkuu wa mkoa Dar es salaam ambaye pia alikua mgeni rasmi, Mheshimiwa
Ezekiel Wenje-Mbunge wa jimbo la Nyamagana pamoja na mkurugenzi mtendaji wa Uchumi
Afrika mashariki Bw. Jonathan Ciano
Bi. Elizabeth Robert ambaye ni mkazi wa manispaa ya
kinondoni, Dar es Salaam aliyefanya manunuzi yake tarehe 22/12/2014 katika duka
kubwa la Uchumi tawi la Shekilango ndie aliyeibuka mshindi wa hisa za Uchumi supermarket zenye thamani ya Tsh
5,000,000/= baada ya kushiriki mara kwa mara katika promosheni hiyo iliyodumu
miezi 3.
Mapema baada ya kuwaalika wageni mbalimbali
wakiwemo waandishi wa habari katika hafla hiyo, ambapo pia ndio ilikuwa siku ya
kuzindua rasmi tawi la Mbezi-Kawe lililopo maeneo ya mbezi chini karibu na
klabu ya kijamii ya rainbow, mkurugenzi wa Uchumi supermarket Tanzania Bw. Chris Lenana alisema “Kupitia shughuli
zetu za kila siku, matawi yetu 5 sasa yanalipa kodi ya serikali kiasi cha millioni
600 kwa mwaka tofauti na mwanzo milioni
50 kwa mwaka tulipokuwa na tawi moja tu”.
Bw. Lenana aliendelea kusema kuwa hadi hivi sasa
Uchumi ina wafanyakazi 430 na imekua mstari wa mbele kabisa katika kukuza ajira
kwa vijana sambamba na kuboresha mishahara ya wafanyakazi wake kila mwaka.
Uchumi pia imekua ikiwajibika kusaidia jamii ambapo kwa kushirikiana na Amref
wameweza kuchangia afya ya mama na mtoto. Hii ilidhihirika kwenye kampeni ya
Simama kwa ajili ya akina mama wa Tanzania ilioanzishwa na AMREF kwa
ushirikiano na Uchumi supermarkets.
Mkurugenzi mkuu wa maduka yote makubwa ya Uchumi
Afrika mashariki Bw. Jonathan Ciano ambaye nae alipata nafasi ya kuzungumza
alisifu maendeleo ya ukuaji mzuri wa maduka hayo makubwa na kusisitiza kuwa
ulipaji ushuru ni kujitegemea akisihi makampuni mengine yaige mfano huo.
Kwa upande mwingine
Mheshimiwa Said Meck Sadik ambaye ndiye alikua mgeni rasmi wa hafla
hiyo, alishukuru kwa kukaribishwa ili kuweza kuzindua duka hilo kubwa na kusifu
ubora wa huduma na bidhaa za Uchumi na kuwahasa kuendelea hivyo hivyo.
“Bado sijaridhika na matawi matano tu, ninamatumaini
makubwa kuwa mnaweza kwenda zaidi ya hapo” alisema Mheshimiwa Sadik. Aliyataja
baadhi ya maeneo ambayo yana wingi wa watu kama Kibaha, Mbagala na Kigamboni
akitolea mfano kuwa hayo ni maeneo wanayoweza kuwekeza ili watanzania waendelee
kufaidika na huduma zao. Alitaja baadhi ya miji kama Mbeya, Mwanza na Arusha
ambapo pia kuna fursa nzuri za biashara na wingi wa watu. “Dhumuni lenu liwe ni
kuifikia angalau asilimia 60 ya watanzania wote hapa nchini na kutokana na hilo
hata uchumi wa nchi hii utapata afya”…alimalizia Mheshimiwa.
Aliendelea kuwahasa watanzania wanaopewa nafasi kazi katika
makampuni kama haya ya kigeni kuwa waaminifu, kuchapa kazi kwa bidii na kuacha uzembe unaojitokeza kila mara na kisha
kubaki kulalamika tu.
Ni takribani miaka minne sasa tangu Uchumi ianze
kufanya biashara hapa nchini. Kampuni hiyo imekuwa na utaratibu wa kuwazawadia
wateja wake kila mwisho wa mwaka na kwa mwaka huu Uchumi wameenda mbele zaidi
kwa kutaka kuwafanya wateja wawe wamiliki halali wa kampuni hiyo tofauti na
mwanzo ambapo zawadi zilizotolewa kama ni kama seti ya fanicha, Jiko Bab Kubwa na
talii na uchumi.
Kipindi hiki
waliamua kuanzisha Mimi mwanahisa promosheni ambapo lengo la promosheni ni
kumpata mshindi ambae angekuwa mmiliki wa Uchumi kupitia hisa (amana) zenye
gharama ya Tsh. Milioni 5.
Promosheni hii ilianza rasmi tarehe 25 No 2014 na
ilitakiwa kuifikia kikomo tarehe 15 Januari 2015 ambapo kipindi chote hiki
mteja alitakiwa kufanya manunuzi ya bidhaa zenye jumla ya Tsh 20,000 na hapo
basi angeingizwa kwenye droo ili kujaribu bahati yake nasibu ya kushinda zawadi
mbalimbali zilizoorodheshwa na Uchumi hapo awali. Sambamba na zawadi ya hisa
kwa mshindi mkuu, zawadi nyingine zilizoshuhudiwa zikitolewa ni kama
ifuatavyo:- T.V bapa ya LG (Flat screen), Microwave, Water dispenser, Simu ya
mkononi aina ya Techno H3, Ofa ya kufuliwa nguo kwa mwaka mzima, Chakula cha
jioni kwa wapendanao watatu katika hoteli ya Serena Hotel ada za shule kwa
watoto zenye thamani ya Tshs 600,000/=, vocha za manunuzi zenye thamani ya
shilingi Tshs 720,000/= zitakazo tumika nchi nzima kwa kipindi cha mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment