1.
Nakupenda: Ni kitu rahisi na cha wazi cha kumwambia mpenzi wako.
Hakikisha tu kuwa unamaanisha. Jaribu kulisema neno hilo pindi mpenzi
wako anapokuchekesha au pale anapofanya kitu kinachokukumbusha kwanini
mko pamoja.
2. Nilikuwa nakuwaza: Ni muhimu kumjulisha mpenzi wako kuwa unamuwaza hata kama hamko sehemu moja.Ukiona kitu kizuri au cha kuchekesha katika siku yako ambacho kinakufanya umkumbuke, mjulishe.
3.
Siku yako ilikuaje?: Muulize masuala ambayo mpenzi wako anakutana nayo
katika shughuli za kila siku. Muulize kuhusu huyo mfanyakazi mwenzie
anayemkera au kazi kubwa waliyokuwa wakifanya. Kumpa nafasi mpenzi wako
kushare sehemu zingine za maisha yake kutasaidia kuunganisha dots kati
ya muda mnaokuwa pamoja.
4.
Unga mkono maamuzi mazuri ya mpenzi wako: Mpe moyo mpenzi wako kwa
kumjulisha kuwa unaunga mkono maamuzi yake. Unaweza ukaenda mbali zaidi
kwa kujaribu kumsaidia afanikishe malengo aliyojiwekea. Maisha yamejaa
vikwazo vingi, na ile hisia kuwa una mtu mwingineupande wako zinaweza
kukusaidia kuvivuka. Msiwe couple tu, kuweni timu. Kumkumbusha mpenzi
wako kuwa upo nyuma yake kutaimarisha uhusiano wenu.
5.
Mwambie mpenzi wako kuwa Umependeza: Kama umekuwa kwenye uhusiano kwa
muda mrefu, ni rahisi kujisahau katika mengi. Ni muhimu kumkumbusha
mpenzi wako kuwa anakuvutia. Kumjulisha kuwa ‘gauni hilo limekupendeza
sana’ kutamfanya ajisikie vizuri na kukumbusha kwanini ulimchagua yeye.
6.
Samahani ni neno zuri kwa mpenzi wako: Kila mtu hukosea wakati fulani.
Wakati mwingine hujikuta tukiongea maneno kwa hasira na baadaye kugundua
kuwa hatukuwa sahihi. Ubishi hauna nafasi kwenye uhusiano wenye furaha,
hivyo omba msamaha unapofanya kosa. Omba msamaha kwa kukasirika. Omba
msamaha kwa kuumiza hisia za mpenzi wako. Omba msamaha hata kwa vitu
ambavyo sio kosa lako.
7.
Hakuna kama wewe: Mpenzi wako anatakiwa kuwa rafiki yako. Kama hautaki
kutembea naye, basi hamkupaswa kuwa kwenye uhusiano. Mfanye mpenzi wako
ajue kuwa yeye ni bora na hakuna kama yeye.
8.
Napenda mawazo yako Picha: StudioMwambie mpenzi wako kuwa unapenda
mawazo yake. Mjulishe kuwa unaona anaakili, mcheshi, anajua kupenda na
ana kipaji.
9.
NakuheshimuKama ulivyo uhusiano wa marafiki, heshima ni kitu muhimu
kwako na mpenzi wako. Mpe nafasi ya kukushauri au kukupa mawazo kwenye
mambo yanayokutatiza. Mtu anapohisi anaheshimiwa, hujisikia pia furaha
na salama, vitu ambavyo ni muhimu kwenye uhusiano wowote mzuri.
10.
Napingana na hilo: Sehemu moja wapo ya kumheshimu mpenzi wako ni
kumjulisha pale usipokubaliana naye. Hakuna mtu anapenda kuoa mtu
anayekubaliana na kila kitu na hakuna mwanamke anayetakakuzaa watoto na
mwanaume asiye na msimamo. Mnaweza kuwa timu, lakini nguvu ya timu
yoyote ipo kwenye mawazo na matendo ya kila mmoja.
Kuwa
na maoni yako na yaseme kwa mtindo wa heshima. Kumpa mpenzi wakomtazamo
tofauti kunaweza kumsaidia kupata suluhisho kwa tatizo ambalo hakuwa
ameliwaza.11. Usiku mwemaTunaishi kwenye wakati ambapo mawasiliano ni
rahisi mno. Kwa kubonyeza tu kitufe tunaweza kutuma ujumbe kuvuka
bahari, hivyo hakuna kisingizio cha kushindwa kusema ‘usiku’
mwema.Haimjulishi mpenzi wako tu kuwa unataka kulala, bali pia
inamjulisha kuwa unamfikiria. Hata kama hamjaongea siku nzima na hasa
kama mmejibizana,
No comments:
Post a Comment