Msanii wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.
Na Mayasa Mariwata/UWAZI
MSANII wa
filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ na aliyekuwa mpenzi wake wa
muda mrefu, Ruta Maximilian Bushoke wamemwagana na hakuna cha ndoa tena.
Akizungumza na Uwazi, Kabula alitoa ya rohoni na kusema kuwa wamefikia
hatua hiyo baada ya kuona mwenzake haoneshi msimamo katika mkakati wao
wa kuoana hivyo kwa sasa wamebaki kuwa marafiki wa kawaida tu kwa sababu
wote ni wasanii.
“Tumeshaachana, mwaka huu nimeuanza kwa kuwa bize na mambo yangu mengine
ya kikazi siyo mapenzi tena. Tulikuwa tumepanga vizuri kwamba tutaoana
na kuamini hivyo kwa kipindi chote alichokuwa nchini Afrika Kusini.”
“Baada ya mwenzangu kutua
Bongo, hakuonesha dalili yoyote ya kutekeleza hilo suala la ndoa.
Sikuwa na uwezo wa kusema nimfunge kamba ndiyo nimlazimishe kumpeleka
kwetu tuoane, nimeona bora niachane naye kwani nimeshachoka na maisha ya
uzinifu nahitaji kuingia katika ndoa,” alisema Kabula.
Bushoke alipotafutwa
kwenye simu hakupatikana lakini kwa mujibu wa marafiki zake wa karibu
wanasema kuwa amesharudi Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment