Makala: Shani Ramadhani
Leo hii kwenye Live
Chumba cha Habari tunaye mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots
2014, Idris Rashid Sultan ambaye amekuwa ndiyo habari ya mjini sasa hivi
baada ya kujishindia kitita cha shilingi milioni 510 na kuahidi
kurudisha nguvu zote kwa Waafrika ambao wamebadilisha maisha yake.
Katika mahojiano na safu hii ambayo huwa inarushwa kupitia Global TV
Online kwenye Kipindi cha Mtu Kati, Idris alifunga zaidi;Mwandishi:
Uliianzaje safari yako ya Big Brother?
Idris: Siku ya usahili nilifika mapema pale New Africa Hotel, namba
yangu ya ushiriki ilikuwa 49 na washiriki tulikuwa wengi sana.
Nikafanikiwa kumaliza awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu nikatakiwa
kwenda Afrika Kusini. Ikafika siku ya kwenda nikaenda, nikafanya usahili
tena nikarudi kusubiria majibu na baada ya wiki mbili-tatu hivi Mungu
alibariki nikachaguliwa kwenda na mwisho wa siku nikashinda.
Mwandishi: Je, ni vigezo gani vilikufanya ukachaguliwa na kuwa mshiriki?
Idris: Ni kigezo kimoja
tu ambacho mimi naweza nikasema kinajumuisha vigezo vyote ni kuwa wewe
kama wewe, naamini ukichaguliwa kwenye usahili majaji wanataka muonekano
wa aina fulani ambao utakufanya uwe mshiriki na ukifika kule usije
ukaonesha kitu kingine tofauti, onesha kilekile ambacho ulikifanya pale
kwa kuwa wewe tangu mwanzo na hicho ndicho kilichonifanya nikashinda.
Mwandishi: Kwa nini watu wakifika kule huwa na muonekano tofauti na maisha yao halisi?
Idris: Hivyo vitu
vinatokea na huwa vinatokea wiki za mwanzo watu wanakuwa na muonekano
tofauti kwa sababu kila mtu anafikiria anahitaji kuwa na muonekano wa
aina fulani ili aweze kubadilika.
Mwandishi: Ulikuwa unalichukuliaje suala la kuoga mchanganyiko?
Idris: Muda wa kuoga ni
mmoja ni namna ambavyo tulikuwa tunajipangilia wenyewe kuwa waanze
wanaume au wanawake na haikuwa lazima kuingia pamoja na unachokifanya
ndani ya nyumba ni juu yako wewe mwenyewe kama ulivyoamua.
Mwandishi: Una mipango ya kufanya kazi Hollywood?
Idris: Nina ndoto kubwa
ya kufika huko, nilivyofika kwenye ile nyumba nilikuwa nina kipaji cha
kucheza lakini pia naamini niko vizuri kwenye uigizaji hata kutoka kwa
Fig, Big, washiriki wenzangu, mwalimu mwenyewe anashangaa kwa hiyo
ninahitaji kuendeleza hicho kitu.
Mwandishi: Mlikuwa mnaishi vipi ndani ya nyumba, na je, kuna mafunzo yoyote ambayo mlipewa kabla?
Idris: Hakuna mafunzo,
ukishafika kule kila mmoja anapewa sheria yenye listi ambazo
zinajulikana labda hutakiwi kuharibu vifaa vya ndani ya nyumba na vurugu
hazihitajiki, vyote mnapewa na kusoma ndani ya wiki moja na hivyo vitu
ndivyo tunaenda kuvifanya kule.
Mwandishi: Vipi kuhusu uhusiano wako na msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’?
Idris: Mimi ni mpiga
picha na msanifu kurasa, Lulu alikuwa anakuja nampiga picha na ni rafiki
ambaye tumejuana kwenye kazi tu, sitaki kujua amejiwekaje
No comments:
Post a Comment