Mzoga wa mamba mwingine. Mzee aliyewatega mamba hao (aliyeketi) akiwa nyuma ya mzoga wa mamba mmojawapo. Mwanakijiji akiweka pozi juu ya mzoga wa mamba kuonesha furaha yake.
WANAKIJIJI wa
Kome-Mchangani wilayani Sengerema mkoani Mwanza, wamewaua mamba wawili
wanaodaiwa kuua watu wawili na kuwajeruhi watu watatu.
Mamba hao waliokuwa katika kingo za Ziwa Victoria kijijini hapo,
walitajwa kuwa kero kubwa kiasi cha kusababisha baadhi ya shughuli za
kuinua uchumi katika kijiji hicho kama vile uvuvi na umwagiliaji
kusimama kwa muda huku wanakijiji wakiwa na hofu ya kuliwa na mamba hao.
Wakizungumza na mwandishi wetu, wanakijiji hao walidai kuwa mara kadhaa
walifikisha malalamiko yao kwa viongozi wa serikali lakini hakuna hatua
zilizochukuliwa, jambo lililowafanya wachange pesa na kumpa mzee mmoja
ambaye alitumia mbinu za kitaalamu kuwatega mamba hao na hatimaye kuwaua
No comments:
Post a Comment