Mwanamke mmoja nchini Misri ameamua kukatiza na gauni la arusi mitaani kupinga masimango anayokutana nayo kwa kuchelewa kuolewa.
Samah Hamdi mwenye
miaka 27 alifikia uamuzi huo baada ya kuchoshwa na kashfa kutoka kwa
watu wanaomzunguka ikiwemo familia yake hasa mama yake mzazi ambao
wamekua wakimsema kutokana na kutokua na mume mpaka sasa.
Hamdi ambaye ni mwanafunzi wa shahada ya uzamili alisema ameamua
kutembea hivyo mitaani na kamwe hawezi kuacha dhamira yake hiyo ikiwa
kama ishara ya kupinga mila na desturi inayowakandamiza wanawake
wasioolewa.
No comments:
Post a Comment