Coutinho alifunga bao hilo dakika ya 86 kwa shuti kali akimalizian krosi ya beki wa kulia, Juma Abdul.
Yanga SC inamaliza kwa ushindi wa asilimia 100, ikishinda mechi zake zote tatu za Kundi A, 4-0 mara mbili dhidi ya Taifa Jang’ombe na Polisi na leo 1-0.
Yanga SC, sasa itamenyana na JKU ya Zanzibar katika Robo Fainali keshokutwa usiku, hapa hapa Uwanja wa Amaan.
Yanga SC ilicheza vizuri kipindi cha kwanoutiza na kutawala mchezo, lakini washambuliaji wake Mrisho Ngassa, Danny Mrwanda, Simon Msuva na Andrey Coutinho walikosa mabao ya wazi.
Kilichowakosesha mabao Yanga SC kipindi cha kwanza ni kukosekana kwa ushirikaino baina ya watu wa mbele, kutokana na kila mchezaji kutaka kufunga mwenyewe badala ya kumpa aliye kwenye nafasi nzuri zaidi.
Hali hiyo ilisababisha wachezaji hao waanze kulaumiana kwa kunyimana mipira kwenye nafasi.
Kipindi cha pili, Yanga SC waliendelea na kosa kosa langoni kwa JKU, kiasi cha mashabiki wake kuingiza imani za kishirikina wakiamini kipa wa Shaba ameweka uchawi langoni mwake.
Katika halli isiyo tegemewa Mashabiki wa timu hiyo walivamia kwenye lango la Shaba na kubeba glavu za akiba za kipa wa timu hiyo, Bakari Shaweji na kwenda kuzitupa nje ya Uwanja.huku imani ya kishirikina zikidaiwa dakika kumi baadaye Yanga ilipata bao dakika ya 86 kupitia kiungo wake Mbrazili Adrey Countinho
Hata hivyo, mashabiki wawili walikamatwa na Polisi na kupelekwa kituoni.
Kwa matokeo nayo, Yanga SC itamenyana na JKU katika Robo Fainali keshokutwa usiku Uwanja wa Amaan, mchezo ambao utatanguliwa na mechi kati ya KCCA na Polisi Saa 9:00 Alasiri, Azam FC na Mtibwa Sugar Saa 11:00.
Robo Fainali ya kwanza itachezwa kesho Saa 2:15 Usiku Uwanja wa Amaan, kati ya SImba SC na Taifa ya Jang’ombe.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Edward Charles, Rajab Zahir, Kevin Yonean, Said Juma ‘Kizota’/Salum Telela dk59, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Hassan Dilunga dk81, Danny Mrwanda/Kpah Sherman dk59, Mrisho Ngassa/Amisi Tambwe dk59 na Andrey Coutinho.
Shaba FC; Bakari Shaweji, Robert Daniel, Juma Mwalimu, Bakari Kidarusi, Hassan Shaaban, Shekha Khamis, Kassim Kiondo, Suleiman Ally, Said Sinde, Mohammed Nyasa na Hamisi Ramadhani/Suma Ozil dk83
No comments:
Post a Comment