02 December 2014

HUJAFA HUJAUMBIKA: “BILA NYINYI WATANZANIA, MIMI NAKUFA”


Hajira Twalib Mdoka akiwa mwenye maumivu makali baada ya kuugua ugonjwa wa kansa. Hivyo ndivyo alivyoanza kusimulia mtoto Hajira Twalib Mdoka,17, (pichani), mkazi wa Mbezi Msigani,wilayani Kinondoni jijini Dar ambaye kwa kipindi cha miaka 16 amekuwa mgonjwa. “Hali niliyonayo kiafya kwa sasa ni ya kutia mashaka, sina muda mrefu kuendelea kuishi hapa duniani, nikifikiria ninavyoteseka ndani ya familia yangu nikichanganya na maumivu ya ugonjwa usiopata matibabu, naamini bila msaada wenu nitafariki dunia.” 
NINACHOUGUA
Amesema ugonjwa unaomsumbua ni kansa, anajisaidia katika ndoo na kubebwa na baba yake baada ya kile alichodai mama yake kumkimbia.Alisimua jinsi anavyotaabika kama ifuatavyo:
“Mimi ni mtoto wa pili kuzaliwa kati ya watoto watatu, nilizaliwa bila tatizo lolote, nilipendwa na wazazi wangu hasa mama alikua kipenzi changu kuliko baba, leo hii mama kanikimbia ninatunzwa na baba ambaye anateseka kwa ajili yangu, najisikia vibaya anavyohangaika nami wakati hana kazi. 

“Wakati nazaliwa wazazi wangu walikuwa wakiishi Mabibo CCM, Dar, baada ya kutimiza mwaka mmoja nilianza kutokwa na mabakamabaka miguuni kisha mwili mzima, utosini kukatokea kidonda baadaye vikaanza kuenea kichwani,vilianza kutoa funza, baba alinichukua hadi Hospitali ya Muhimbili, hapo sasa nikiwa na akili na kujijua. SOMA ZAIDI>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname