21 November 2014

X WA DIAMOND PLATINUMZ PENNY AFUNGUKA KUHUSU MAHARI YAKE, VIMINI, WEMA NA MAMBO KIBAO USIYOYAFAHAMU!

Jina la Penny limo katika orodha ya mastaa waliowahi kuwa na uhusiano na msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’. Jina lake kamili ni Penniel Mwingilwa. Huyu ni Mtangazaji wa Radio Efm ya jijini Dar.
Mtangazaji wa Radio Efm ya jijini Dar Penniel Mwingilwa.
Wiki hii yuko hapa kujibu maswali ambayo waandishi wetu Imelda Mtema na Hamida Hassan walimuweka mtu kati.Ijumaa: Mambo Penny, naona sasa hivi una gari nyingine, ile Toyota Brevis ambayo mpenzi wako wa zamani Diamond alikununulia iko wapi?
Penny: (Kicheko)...kwa kweli namshukuru kwa kuninunulia ile gari ila sasa hivi siko nayo, nimeamua kubadilisha, si unajua mtu lazima uende na wakati?
Ijumaa: Mara ya mwisho kupanda daladala ilikuwa lini?

Penny: Nakumbuka ilikuwa mwaka 2008. Nilipoanza tu kazi ya utangazaji, nilipopanda daladala watu walikuwa wananishangaa sana nikaona hiyo siyo poa, nikawa napanda teksi.
Ijumaa: Ulikuwa na Diamond mkaachana, hebu tuambie kwenye maisha yako ungependa umpate mwanaume wa aina gani?Penny: Kwanza awe mchamungu, pili anithamini lakini pia awe mtu muelewa. Yaani ajue ni wakati gani wa kufanya maamuzi sahihi na awe tayari kunisikiliza.
Ijumaa: Nini ambacho kinakukwaza sana na hukipendi kabisa?

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname