20 November 2014

WEMA AANIKA KISA CHA KUMMWAGA DIAMOND


MISS Tanzania 2006/07 ambaye ni staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’, amevunja ukimya kwa kuamua kuanika kisa cha yeye kummwaga aliyekuwa mwandani wake, nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
 
Miss Tanzania 2006/07 ambaye ni staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akipozi..
Akizungumza na Amani katika mahojiano maalum jijini Dar, juzikati, Wema alianza kwa kufunguka kwamba, kuna watu wamekuwa wakizungumzia ishu ya yeye kumtema Diamond huku kisa wakiwa hawakijui na wengine wamehamishia sababu kwa nyota wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’, jambo ambalo si kweli.
Wema alimwaga ‘ubuyu’ kwamba, yeye ameamua kumpa likizo ndefu Diamond ili kila mmoja aweze kufanya mambo yake ya maana kwa uhuru mkubwa hasa baada ya jamaa huyo kunukuliwa na magazeti pendwa akisema hana mpango wa kuoa jambo ambalo lilimkatisha tamaa na kumwacha njia panda.SOMA ZAIDI>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname