10 . Snoop Lion ($135 million)
juzi kati alikua anaitwa Snoop Dogg lakini kwasasa yupo katika
harakati za kubadilika kuwa msanii wa miondoko ya reggae huku bado
akiendelea kuingiza pesa kutokana na shughuli mbalimbali kama album
sales, touring na mikataba ya kibiashara.
09. Lil Wayne ( $135 million)
Rapper huyu kutoka Cash Money Records amemake kwenye list hii japokua
hutumia pesa nyingi kulipa faini mahakamani. Wayne pia anaingiza pesa
kutokana na record label yake ya Young Money.
08. Ice Cube ($140 million )
Ice cube ni rappper , actor na producer. Ice Cube ametoka kua West
Coast gangsta rap hadi kua katika list ya most powerful people in
Hollywood today.
07. Eminem ( $160 million)
Eminem ni multi-platinum selling hip-hop artist. Mwaka 1997
aliachia album yake ya The Slim Shady EP ambayo ilimfanya Dr. Dre
amchukue na kufanya kazi naye kazi. Utajiri wake unatokana sana na
muziki anaoufanya.
06 . Birdman ($170 million)
Mmoja kati ya wamiliki wa record label ya Cash Money ingawa
kilichomfanya awe katika nafasi hii ni mauzo ya kinywaji chake aina ya
Vodka.
05. 50 Cent ($270 million)
50 ni rapper na mjasiriamali pia. 50 amepata utajiri wake kutokana
na mikataba ya kibiashara aliyonayo na mauzo ya nyimbo zake. Tokea
alipotoka kwa mara ya kwanza na album yake ya Get Rich or Die Trying ,
50 amekua katika list hizi ever since.
04. Master P ( $350 million )
Master P ni mkogwe wa Rap, Mjasiriamali na film producer pia. Miaka
ya 1990 , jamaa alijenga hekalu lake la biashara. Hekalu lililohusisha
rap labels mbalimbali, clothing line , management company , travel
agency , film production company na video production company.
03. Dr. Dre ( $450 million )
huyu ni rahisi kuelezea. Tengeneza headphones set za quality ya
kawaida, pandisha bei yake kwa asilimia 900 na kisha wape watu maarufu
wazivae na kuuza nazo sura. Hapa ndipo patawafanya watu kutaka kuhisi
muziki wa headphones hizi na mwisho kumtajirisha Dr. Dre
02 . Jay Z ($550 million )
Anaweza asiwe wa kwanza lakini bado dola millioni 43 za kimarekani ni
bonge la mkwanja !! Akiwa ni mfanyabiashara halisi, Jay Z kawaida
ufikiria kitu kipya. Dili la dola za kimarekani milioni 5 alilosign na
kampuni ya samsung imemuongezea pesa nyingine zikiwe ni mauzo ya
kinywaji chake cha Armand De Brignac .
01 . P. Diddy ( $650 million)
Hii inakuaje ? P. Diddy hajasikika tokea alipobadilisha jina lake
kuwa la kitoto. Kinywaji cha Ciroc vodka ndio kimempa ulaji. Diddy
anaweza akashukuru kupata pesa nyingi kutokana na mafanikio ya kinywaji
chake na pia record label yake ya Bad boy na clothing line yake ya sean
Jean ambayo iliuza sana kipindi cha zamani.
Usidhani tumesahau kwamba hii ni top 20, basi wengine walioshika
namba 11 hadi ishirini ni hawa hapa na utajiri wao kwenye mabano.
11. Kanye West ($120 million )12. Pharrell Williams ( $110 million )
13. LL Cool J ($100 million)
14. Timbaland ( $85 million )
15. Akon ($80 million )
16. Beastie Boys ( $75 million kila mmoja )
17. Nelly ($60 million)
18. T.I. ($50 million )
19. Pitbull ($50 million )
20. Nicki Minaj ($45 million)
21. Andre 3000 ($45 million )
22. Drake ( $40 million )
23. Ice-T ($40 million )
24. Big Boi ($40 million )
25. T-Pain ( $35 million )
26. Rick Ross ($35 million )
27. Busta Rhymes ($30 million )
28. Flo Rida ( $30 million )
29. Ludacris ( $25 million )
30. Chris Brown ( $24 million
No comments:
Post a Comment