16 November 2014

SHEMEJI YETU KWA JOKATE HUYU HAPA!!!

Mwanamitendo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amemwanika mwanaume mpya mtandaoni huku wakiwa wamepozi katika staili ya wapendanao.

Awali, paparazi wetu alitonywa na sosi aliyeomba hifadhi ya jina lake kuwa amemuona mwanaume mpya wa Jokate katika mtandao wa Instagram.

“Nimemuona Jokate na mwanaume wake mpya lakini simjui kwa jina, kama huamini ingia kwenye mtandao wa Instagram uone mtoto wa kike alivyojiachia katika pozi za kimahaba,” alisema sosi huyo.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu aliingia kwenye kilongalonga chake na kuperuzi katika mtandao huo kisha kujionea picha hizo, haraka sana akazisevu katika simu yake.

Aidha, wadau mbalimbali waliopo katika mtandao huo walitoa maoni mbalimbali huku wengi wao wakimpongeza.

Baada ya paparazi wetu kuzitia kibindoni picha hizo, alimsaka Jokate kwa njia ya simu ili azitolee ufafanuzi.

Mwandishi: Haloo Jokate…

Jokate: Nitumie meseji nipo kwenye kikao.

Mwandishi wetu alimtumia meseji kama alivyoshauri staa huyo ambapo alimtaka amtambulishe mwanaume huyo na aeleze kama ndiye mpenzi wake mpya, hakujibu chochote.

Paparazi wetu alimtumia meseji ya pili kumsisitiza atoe majibu ndipo alipojibu kwa kifupi:“Hapana mumy!”

Pamoja na majibu hayo, paparazi wetu alimtumia meseji nyingine kumuuliza kama siyo mpenzi wake ni nani lakini hadi tunakwenda mitamboni, hakujibu chochote.

Kabla ya kumuanika mwanaume huyo, Jokate aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku pia akitajwa kutoka na mcheza kikapu, Hasheem Thabeet

1 comment:

  1. The wonderful benefits of Brazilian hair extensions are not only restricted to the A-rated celebrities and for the red carpet, they can also be experienced by the general public and have grown as a symbol of modernization. brazilian hair sale The long and natural hair proxy posses an outermost protective layer, which forms as a covering, called as a cuticle layer. brazilian hair uk The unidirectional nature of the cuticle layer shows the natural light which directly falls on the hair. brazilian hair The expression of natural lights adds the luster and glamour of the hair proxy. In addition with providing luster to the hair, the cuticle layer is responsible in increasing the charge lifespan of the proxy.

    ReplyDelete

Comments system

Disqus Shortname