16 November 2014

MWANAUME MCHAPAJI MWENYE VIDOLE 12 MIKONONI AENDA KUSAKA AJIRA UINGEREZA..

Vijay akionesha vidole vyake 12 vya mikono.
Mchapaji wa India Vijay Singh anaweza kuchapa zaidi ya maneno 100 kwa dakika kwa kutumia vidole vyake 12.

Lakini Vijay, ambaye pia ana vidole 12 vya miguuni kutokana na dosari yake hiyo ya kimaumbile, anasema hawezi kupata kazi katika nchi yake aliyozaliwa sababu waajiri wanataka tu wanawake wenye mvuto.
Sasa anapanga kuhamia Uingereza kwa lengo la kutafuta ajira baada ya kuwa amekataliwa maombi yake ya kazi zaidi ya 50.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 48, anayetokea Agra kaskazini mwa India, alisema: "Wanataka wanawake wenye mvuto, si wanaume wenye vidole 12."
INAENDELEA>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname