Mwanzilishi
wa mtindo wa TAKEU ambao haupo tena, Lucas Mkenda aka Mr Nice
amekanusha kuwa ulevi na mademu ndio unaosababisha ashindwe kutulia na
label moja ya muziki.
Mr Nice akiwa kwenye nyumba yake iliyopo Kibamba jijini Dar es salaam
Mr
Nice amesema label nyingi zinashidwa kuelewana naye kutokana na wao
kuhitaji sehemu kubwa katika kinachopatikana pamoja na kumnyima mamlaka
kama msanii mkubwa.
“Tumeshindwana
kwa sababu ya utawala kwa sababu ukiangalia mikataba yangu yote wao
ndo wanataka wawe mabosi, kitu ambacho kwangu hakiwezekani,” Nice
ameiambia Bongo5. “Halafu unataka uni-meneji wakati kabla wewe kukutana
na mimi nilishakuwa na kazi zangu nyingi ambazo bado zinahitajika.
Wakati mimi bado nina jasho langu la Kikulacho, la Fagilia, album zangu
ambazo mimi nimefanya mimi mwenyewe kwa jasho langu nikajipromoti
mwenyewe iweje unimeneji halafu utake kupata asilimia kutoka kwenye
jasho langu? Huoni huo ni wizi wa wazi wazi?
Candy
& Candy mimi niliwaambia kazi yangu inaendelea kubaki kazi yangu
ile ya nyuma, kama mnataka tutafanya project mpya ndo tutaongelea
suala la percent gani mtapata kutokana na promotion mtakayoifanya
lakini hamna uwezo wa kusimamia kazi yangu yote ambayo niliifanya kwa
jasho langu. Kama niliweza kufika hapa nilipo sasa nahitaji menejimenti
ya nini? Mbona niliweza kujitoa toka huko nilipokuwa mpaka nikafika
hapa?,” amehoji.
“Mimi
nadhani mikataba iliyovunjika ni miwili na sababu za kuvunjika
zinafanana.. Nakumbuka nilikuwa na mkataba na akina Lamar tukashindwana
hapo kwenye suala la nani ni nani katika mkataba, basi tukasema tuache
mkataba mpaka uishilie huko. Nikafanya mkataba na GrandPa Records
Nairobi ambayo nao tulishindwana kwa sababu hizo hizo. Unajua mara
nyingi unaposhindwana mikataba na hawa watu wanazusha chochote. Sijui
jamaa hataki kunisikiliza, jamaa anafanya hizi lakini ukweli unakuja
pale pale, mameneja wanataka uwafuate wao wanataka nini, Mimi ninaimba
muziki wa watoto wa uswahilini inakuwaje unataka nikawaimbie watoto wa
Masaki? Mimi nadhani mameneja wengi wanakuwa wasanii kufanya vitu kwa
mitazamo yao bila kuangilia na malengo ya msanii binafsi.”
No comments:
Post a Comment