19 November 2014

MAKAVU LIVE: ALIKIBA KUMBUKA MAJIVUNO, MARINGO NDIVYO VILIVYOKUPOTEZA!


Kwako

staa uliyerudi kivingine na wimbo wa Mwana, Ali Kiba. Vipi uko poa? Bila shaka u-mzima wa afya na unaendelea na harakati zako za kimuziki.Ukitaka kujua hali yangu, mimi ni mzima wa afya namshukuru Mungu maisha yanasonga. Naendelea na majukumu ya kila siku likiwemo hili la kukuandikia barua. 
Pasipo kupepesa macho, pamoja na salamu, dhumuni la kukuandikia barua hii ni kwamba kuna kitu kimenigusa nataka kukukumbusha maana akili ya mwanadamu siku zote imeumbwa kusahau. 
Ni rahisi sana mtu kula msoto mkubwa lakini ndani ya dakika chache tu pale unapopata mafanikio, unasahau.Nakumbuka kabla ya kuachia nyimbo za Kimasomaso na Mwana ambazo zinaendelea kufanya vizuri hadi sasa, ulikuwa kimya. Najua unaweza usikubaliane na mimi lakini ukimya ule ulitokana na kujisahau baada ya kuwa na mafanikio makubwa. 


Kipindi kile ulifanikiwa kuiteka Bongo, kila mmoja alikuwa akikutambua wewe kama namba moja hususan pale ulipofanikiwa kuwa msanii pekee kutoka Tanzania na kwenda kufanya kolabo maalum iliyoandaliwa na legendary wa muziki kutoka Marekani, R. Kelly. SOMA ZAIDI>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname