26 November 2014

HAIJAWAHI KUTOKEA: MAZISHI YA BILIONEA WA MAPENZI GARINI BUKOBA HISTORIA!

Msafara wa magari kuelekea kwenye mazishi. Tukio hilo la mazishi lilijiri Jumamosi iliyopita katika Kijiji cha Kyaikailabwa, nje kidogo ya mji wa Bukoba ambapo siku hiyo, shughuli zote zilisimama kwa siku nzima kupisha tukio hilo lililogusa hisia za watu wengi.

ACHANA na mazingira ya kifo cha Bilionea maarufu wa Bukoba, Leonard Mtensa aliyefariki saa chache baada ya kufanya mapenzi ndani ya gari kuacha gumzo, gumzo lingine lilitokea wakati wa mazishi yake ambayo yalihudhuriwa na wananchi wengi kutoka ndani na nje ya mkoa, mkanda kamili huu hapa.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia mazishi hayo mwanzo mwisho, msiba huo ulikuwa wa pekee kwani haijawahi kutokea kwa yeyote kuzikwa na umati mkubwa kiasi hicho na kusababisha watu wote wasimame kiasi cha kuwafanya askari wa usalama barabarani kufanya kazi ya ziada kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.
Wananchi wakiwa barabarani kushuhudia msafara huo ukipita. “Msafara ulianzia mochwari ya Hospitali ya Bukoba, ukapita katika klabu yake ya Lina’s kisha ukapitia mtaa wa Jamhuri lilipo Soko Kuu la Bukoba kisha kuelekea kijiji cha Kyaikailabwa. 
“Ilikuwa si mchezo, hii ni historia kwa Bukoba. Haijawahi kutokea msiba wa mtu wa kawaida ukawasababisha watu kujipanga barabarani, trafiki kuongoza harakati utafikiri mapokezi ya rais,” kilisema chanzo. 
Inadaiwa kuwa msafara wa magari ulivunja rekodi kwani wakati magari mengine yalikuwa yameshafika makaburini, mengine yalikuwa bado kwenye foleni nyumbani. 
Jeneza likibebwa kuelekea makabulini. 

Chanzo hicho kilizidi kupasha habari kuwa, msafara wa kutoka nyumbani kwa marehemu, Bukoba mjini hadi katika Kijiji cha Kyaikalabwa ambacho kipo umbali wa kilomita 3, ulikuwa mrefu kiasi ambacho magari yalijipanga kuanzia mjini hadi kaburini. 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname