Mtangazaji Gardner Gabriel Fikirini Habash ‘Kapteni’ akila ujana na binti (jina halikupatikana mara moja) mrembo bwawani (swimming pol).
JAHAZI linazidi kwenda mrama! Wakati shauri lao la kugawana mali likidaiwa kufikishwa mahakamani, picha mpya imenaswa ikionesha dhahiri kwamba Mtangazaji Gardner Gabriel Fikirini Habash ‘Kapteni’ ameamua kusonga mbele na maisha yake na kusahau kabisa kama alikuwa na mke aitwaye Judith Daines Wambura Mbibo ‘Jide’, Amani linakupa mchapo kamili.PICHA IPOJE?
Picha hiyo ambayo inamuashia ‘endiketa’ Jide kuashiria kwamba, Gardner amejiweka pembeni na kuwa bize na ‘starehe’ zake, inamuonesha mtangazaji huyo akiwa ‘ziro distensi’ na kabinti kabichiii (jina halikupatikana mara moja) katika bwawa la kuogelea (swimming pol) huku wakiwa wamening’iniza miguu kwenye maji.
PICHA ILIVYOVUJA
Kwa mujibu wa chanzo makini, picha hiyo iliibwa katika simu ya binti huyo aliyekuwa na Gardner kisha kuisambaza katika mitandao ya kijamii bila yeye mwenyewe kujua.
“Yule dada aliyekuwa na Gardner aliibiwa picha hiyo na shosti yake katika simu yake ndipo akaisambaza mitandaoni,” kilisema chanzo hicho.
Mara baada ya mapaparazi wetu kunasa picha hizo, kabla ya kumtafuta Gardner ili kujua ukweli, walianza kusaka eneo ambalo wawili hao walikuwa wakiponda raha zao ambapo jitihada hizo zilikosa majibu ya moja kwa moja.
“Hii ilikuwa ni Mikocheni, Escape One siku hiyo kaka mkubwa alikuwa akifanya yake si unajua tena ameshaona liwalo na liwe,” kilisema chanzo cha kwanza.
No comments:
Post a Comment