14 November 2014

DAVINA NIWAPO CHUMBANI NI MWENDO WA NGUO LAINIII!


Mkali katika tasnia ya filamu bongo, Halima Yahaya 'Davina'.
Leo kwenye safu yetu hii tunaye mwanadada kutoka kwenye tasnia ya filamu Bongo anayefahamika kwa jina la Davina lakini jina alilopewa na wazazi wake ni Halima Yahaya.
Kama ilivyo ada naye anajibu maswali 10 yahusuyo maisha yake binafsi na kisanii ambayo paparazi wetu Hamida Hassan alimbana na aliyajibu kama ifuatavyo;
Ijumaa: Najua una dada wa kazi, unapokuwa nyumbani huwa unafanya nini?
Davina: Licha ya kuwa na dada wa kazi, nikiwa nyumbani si mtu wa kukaa tu, napenda kufanya usafi wa nyumba yangu, kupika na kucheza na mtoto.
Ijumaa: Je, ni chakula gani unachopendelea kumpikia mumeo?
Davina: Kiukweli mume wangu anapenda sana makaroni na nyama ya kusaga, ili kumfanya awe na furaha huwa nampikia chakula hicho.
Ijumaa: Ni sehemu gani ya mwili wako unayoipenda zaidi?

Davina: Sibagui, kila sehemu ya mwili wangu naipenda na namshukuru Mungu kwa kuniumba hivi nilivyo.INAENDELEA>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname