Inavyoonekana
siku hizi japo kweli kuna tatizo la upungufu wa nguvu za kiume haswa
kwa mazingira ya mijini, Lakini hili tatizo linaonekana kukuzwa kuliko
lilivyo hadi imepelekea woga mkubwa kwa baadhi ya wengi wetu.
Ndipo
kwenye tafakari yangu nikaona NIANZISHE HUU UZI kwa machache tu kwa
ufahamu mchache nilio nao, Ili NIWAALIKE wengi WENU kwa msaada zaidi wa
mawazo kwa ndugu zetu wanaokutana na mfadhaiko huu.Nikiamini pia
wengi wenu mna utaalamu na mnaoweza kuchambua haya makitu kwa ufanisi
zaidi mkatatusaidia sana kwenye uzi huu. Yafaa sasa tujikite kwenye
ufumbuzi kuliko kuripoti tatizo na kulaumu. Kadiri tunavyoendekeza
kuripoti tatizo tunawaathiri hata wale waliokuwa wazima ambao kwa kuwa
hakuna kipimo sawia kujua kipi ni kipi, nao wasiwasi unawafanya
wanapoteza ujasiri wao na kujiona wana tatizo kumbe wapo imara sana
kuliko mkuki.
Kuuweka Mwili vizuri: Ni
wazi kuwa tendo hili linachagiwa sana na mzunguko mzuri wa damu. Mwili
ukiwa kwenye hali nzuri kiafya na tendo huwa linaenda ipasavyo. Na mwili
ukiwa dhoofu basi tegemea tukio dhoofu pia. Hivyo ukitaka kuwa na
matokeo mazuri kwenye ndoa yako, jitahidi sana kujiweka vizuri kwa kula
sahihi na kufanya mazoezi mepesi mepesi tu kwa wale wanaoweza kuutumia
muda vizuri wapiti pite Gym walau siku mbili na kuendelea kwa wiki.
Kufahamu kuwa kupumzika kwa uume baada ya baada kufika mara ya kwanza sio tatizo. Kwa
wanaume walio wengi, baada ya mshindo wa kwanza hupumzika kidogo kabla
ya kuendelea na awamu nyingine. Japo kuna ambao wana uwezo wa kuendelea
moja kwa moja bila kupumzika (law ya use and misuse inahusika kwa
wengine apa). Kwa hio kusinyaa kwa uume baada ya mshindo wa kwanza,
isifahamike kuwa ni upungufu wa nguvu bali ni ajdustiment ya mwili
wenyewe kutokana na kwamba mwanaume kabla ya tendo mapigo ya moyo
huongezeka na huchangia damu kwenda kwa kasi, na kwa hali hio anakua
yupo juu sana kimhemko, inapofikia anamaliza raundi ya kwanza mwili
unakua unapoa /umesharudi kwenye hali yake
ya kawaida, ndiko kunakosababisha hio maneno kusinyaa kwa wengi wakati
mapigo ya moyo yanaporudi kawaida (MWILI KUPOA).
Maandalizi ya mwili. Wanaume tupo tayari muda wote… ila linapokua swala ya mwenza wako (kwa kuwa muda unaotumia kwa maandalizi na tendo una uhusiano wa moja kwa moja na satisfaction ya mwenzio)… unahitaji muda angalao nusu saa na kuzidi kujiandaa na mwenzi wako. Kama timu ya mpira inapoenda ugenini huhitaji muda kuzoea mazingira,
ndio na mwanaume anavyohitaji muda kuzoea mazingira ya ugenini. Hili
linakusaidia sana mwanaume kutoka kwenye mihemko na kurudi kwenye hali
yako ya kawaida ambayo itakusaidia kuwa na muda mzuri zaidi wa kufurahia
tendo. Jitahidi pia kuvuta pumzi nyingi ndani na uiachie polepole
kukusaidia kukuweka kwenye utulivu mzuri.
Timing ya kuanza tendo:
Kwa kuwa tendo linahusisha sana hisia za mwili, ukiwa umetumia muda
unaotosha kuandaana, basi usiwe na papara mwanzoni, bali uwe na utulivu,
pia jitahidi kuzungumza moja mawili wakati unaanza kuzoea mazingira
mengine (core business) EPUKA UHARAKA na kuweka sana akili yako hapo,
jinafikie mwenyewe kuwa its just a normal thing (mental pride)
Concetration/ Umakini uliopitiliza…
Unapaswa kumfanya mkeo aweke akili yake yote hapo, na wewe unatakiwa
katika kumuweka mkeo kwenye concentration uuharibu umakini wako (level
of concentration). Ukiweka concentration ya juu sana kwenye tendo…
haikuchukui dakika mbili umemaliza, na kuirudisha tena ile hali ya
concentration uliokua nayo mwanzo itakuwia ngumu sana….. Usiweke sana
akili yako hapo kama unataka kufurahia kwa muda zaidi. ila kama hutaki
kudumu.. weka akili na umahini wako hapo woote.. just seconds or a
minute you are done
MAZOEZI ya mwili ni muhimu sana sana sana sana sana kwetu
wanaume. Kama huna muda wa kwenda jimu walau ukiamka piga ‘PUSH-UPS
walau 50’’ kila siku na ‘’SQUARTS’’ . haya ni mazoezi mepesi lakini ni
BORA zaidi kwa mwanaume. Kwetu sisi wanaume tunatumia sana misuli yetu
wakati huu, kwa hio kuna ulazima wa kutafuta ustahimilivu wa misuli
''mussle strength n perseverance''. Hio kitu ni starehe na unatakiwa
baada ya tendo uwe umekuwa refreshed na sio uwe unaumwa kila mahali na
sijui joints zinauma sijui nini nini? ukijiona unakuwa hivyo baada ya
tendo ujue mwili wako haujakaa fiti ipasavyo kimazoezi/kiafya
Pia
Afya ya Akili inahusika sana, Japo inahitaji jitihada makhususi...
lakini kila mtu ana uwezo wa kuchagua nini cha kufikiria na nini si cha
fikiria(kupuuzia) na pia akienda hatua zaidi anaweza kupuuza kila kitu
kwa wakati fulani kama unajua una huo uwezo na ukaamua kuutumia. Pia
kuchagua kufikiri yale yaliopo kwenye uwezo na urefu wa kamba yako
pekee; vitu usivyo na uwezo navyo utajisumbua tu bure na kujipa stress
zaidi. Weka nguvu na jitihada zako kwenye kutafuta ufumbuzi wa
changamoto zako, jifunze na acha kufikiria matatizo kwa maana
hakubadilishi kitu na yataendelea kuwa hivyo n.k n.k................
Ukiwa na namna nzuri ya kuyachanganua mambo yako utasaidika sana kwenye
afya ya akili yako na kuwa vizuri zaidi
Karibuni wadau kusaidia utatuzi wa hili jinamizi linalojizolea umaarufu kadiri siku zinavyokwenda kwenye jamii yetu.
No comments:
Post a Comment