WAKATI nyota wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ akikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa na madawa ya kulevya akiwa njiani kuelekea Mbeya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ aliyekuwa amemfungulia kesi ya kumpiga katika kituo cha Polisi cha Oysterbay, amefuta shauri hilo na kumsamehe.
Ray C maarufu kama kiuno bila mfupa, alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kuandika waraka katika akaunti yake kwenye mtandao wa Instagram, akimsihi Chid Benz kuachana na matumizi hayo ya madawa ya kulevya.
No comments:
Post a Comment