Sakata la umri la Miss Tanzania 2014 Sitti Mtevu limeendelea kuchukua
sura mpya baada ya Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kudai kuwa litamvua
taji hilo endapo watagundua kasoro za umri zinazodaiwa
Akizungumza na gazeti la Nipashe, Katibu Mkuu wa Basata, Geoffrey
Mwingereza , alisema wanasubiri uchunguzi wao ukamilike na wakibaidi
udanganyifu watamvua taji hilo.
Wakati Mwingereza akielezea taarifa
hiyo, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
wanatarajia kukutana leo jijini Dar es salaam kwajili ya kujadili sakata
hilo.
Akizungumza
na gazeti hilo jana, Naibu Waziri wa Wizara ya Michezo, Juma Nkamia
alisema serikali imelisikia sakata la mrembo huyo na wameamua
kuitisha kikao ili kulifanyia kazi.
"Siwezi kukuambia hatua gani
zitachuliwa, ila kesho, (leo) tutakuwa na kikao , serekali haiwezi kukaa
kimya , kuna vyombo vyake vinalifanyia kazi" alisema Nkamia.
Aliongeza kuwa yeye alikuwa nje ya Dar es Salaam lakini kuna maelezo
aliyoyatoa na yameanza kufanyiwa kazi
No comments:
Post a Comment