17 September 2014

TABORA WAMKATAA NUH MZIWANDA…WASEMA HAWEZI KUWA MUME WA SHILOLE

Nuh Mziwanda jana alijikuta katika wakati mgumu mjini Tabora baada ya Shilole kuwauliza wakazi wa mkoa huo anakotokea iwapo Nuh Mziwanda anafaa kuwa mume wake.


Shilole ambaye ni mchumba wa Nuh alifunguka mbele ya mashabiki wa Tabora waliokuwa wamefurika kushuhudia show ya Serengeti Fiesta kutaka kujua kama wanamtaka Nuh Mziwanda awe shemeji yao kitu ambacho mashabiki hao walikataa
Mbaya zaidi kwa Nuh, mashabiki hao walimpendekeza DJ Zero kuwa ndiye mwanaume wanayemtaka awe shemeji yao. Shilole aliwajibu wakazi hao kuwa hata wafanyaje yeye binafsi anampenda dogo dogo wake Nuh.

Nuh ambaye kauli hiyo ya shemeji zake wa Tabora ilimnyong’ozesha magoti, ameiambia Mpekuzi kuwa wale ni mashabiki tu hivyo Shilole ataendelea kuwa mpenzi wake na anatarajia  kumvalisha pete ya uchumba Shilole.

“Unajua mashabiki ni watu na zile kauli walizotoa haziwezi kurudisha nyuma kauli yangu kutompenda Shilole,” amesema Nuh  na  kuongeza:

Bado ni baby wangu, na kuna mambo mengi yatakuja. Ndioa maana baada ya kuona wanapiga kelele nikaamua kuwatuliza kwa pesa na mwishowe mambo yakaenda sawa.
  
 “Unajua ingawa watu wanasema mengi juu yetu kiukweli sisi tunapendana na hivi karibuni nitamvalisha pete ya uchumba.”

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname