MSANII
wa siku nyingi katika tansia ya filamu Bongo, Salama Salmin ‘Sandra’
amefunguka kuwa tangu ameanza kujihusisha na mambo ya sanaa hajawahi
kuwa na bwana ndani ya klabu ya Bongo Movies na wala hajawahi kutoa
rushwa ya ngono kwa ‘dairekta’ kama ilivyo kwa wengine.Msanii wa siku
nyingi katika tansia ya filamu Bongo, Salama Salmin
‘Sandra’. Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Sandra
alisema kuna baadhi ya wasanii wanafikiri kuwa na mwanaume ndani ya
Klabu ya Bongo Movie ndiyo kutimiza ndoto zao kumbe ni kujidharaulisha
tu.
“Sina bwana wala sijawahi kutoa rushwa ya ngono kwa ‘dairekta’ na
sifikirii kufanya hivyo kamwe, maana ni kujishushia heshima yangu wakati
mimi ni mke wa mtu na wala siwezi kunadi mwili wangu,” alisema Sandra.
No comments:
Post a Comment