Muimbaji
wa Tip Top Connection, Madee hivi karibuni alijikuta katika wakati
mgumu baada ya kuwekwa ndani katika kituo cha polisi cha Kigamboni
kutokana na madai ya kuhusishwa na tukio la utekaji.Kabla
ya kuongea na meneja wa kundi hilo, Babu Tale, mtangazaji wa Clouds FM,
Soudy Brown aliripoti kupitia ‘You Heard’ ya XXL kuwa Jumamosi
iliyopita Madee aliporwa simu yake na watu wawili usiku huko Kigamboni
Babu Tale alisema: "Kwenye
mida ya saa tisa usiku Madee wakati anatoka kwenye show Kigamboni kuna
waporaji simu wakiwa kwenye pikipiki wakampora,kwahiyo ikabidi gari
aliyokuwemo Madee ikiendeshwa na Kwebe ianze kuikimbiza ile pikipiki
halafu wakaigonga pikipiki kwa nyuma.
"Pikipiki ilivyodondoka yule aliyekua nyuma kwenye pikipiki ambaye
ndio alipora simu akafanikiwa kukimbia hivyo wakaishia tu kumkamata
aliyekuwa anaendesha hiyo pikipiki.
“Wakamchukua na kwenda nae maskani TipTop,” ameeleza Tale.
Mama yake akaja akasema,"msipeleke polisi mwekeni hapa mi nakwenda
kuwachukulia vitu vyenu. Madee kwa sababu alikua anakwenda kwenye show
Mwanza ikabidi aende zake, saa nne asubuhi yule mama akaja na polisi
badala ya kuja na mwizi, mwenzake akaja na polisi kataka kuwaokota
watoto wote ofisini kwangu pale Tiptop.
" Walimchukua huyo mhalifu kwenye Land Rover mpaka Polisi Magomeni na kubadilisha kibao kwamba huyu mtuhumiwa alitekwa.”
“Alipigwa akaumia hivyo wakamuombea PF3 wakampeleka hospitali.
Nikapigiwa simu na Madee kwamba anatakiwa polisi akaripoti, kufika
kituoni wakakuta ile pikipiki na kukuta yule dogo ndio anafika kutoka
hospitali akawaambia ‘huyu ni mwizi ameiba’ Ikabidi dogo aingizwe ndani
jana akalala pale polisi Magomeni.
“Asubuhi yake Madee akaenda kituoni kama kufuata mhalifu wake na
kutaka simu yake aliyoibiwa, akaambiwa kesi inabidi ihamishiwe
Kigamboni. Saa kumi na mbili jioni ndio Kwebe ananitumia meseji anasema
Madee analalamika mbona humfatilii, nikauliza ‘kuna nini tena’ akasema
wamemuingiza ndani.
"Nikapiga simu polisi Kigamboni ndio wakaniambia kijana wako
tulitaka kumtoa lakini hatuwezi sababu amemteka mtu. Nikapiga simu
kwenye vyanzo vyangu vya msaada tukamtolea dhamana, ni hilo, yataisha
kama yalivyoanza"-Babu Tale
Source:Millardayo

No comments:
Post a Comment