26 September 2014

LULU MICHAEL APANGISHIWA JUMBA LA KIFAHARI NA BILIONEA


Madai mazito ya kushtua mtaani yanasema kwamba staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, mambo yake kwa sasa yapo juu ya mstari baada ya bilionea kutoka jijini Arusha (jina tunalihifadhi kwa sasa) kudaiwa kujitosa kumlea akianza kwa kumpangishia jumba kubwa la kifahari.
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, akiwa na begi la fedha.
TWENDENI USHUANI Habari hizo za mitaani zilidai kwamba bilionea huyo amempangishia Lulu mjengo huo wa maana uliopo ushuani maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Kimuonekano, nyumba hiyo iliyoshuhudiwa na wanahabari wetu mwanzoni mwa wiki hii haina tofauti na ile mijengo iliyozoeleka ya mastaa wakubwa wa Marekani kwa maana ya kujitosheleza kwa kila kitu ndani yake.
Kwanza ni nyumba yenye fensi kubwa na kuingia getini lazima ujieleze ‘vizuri’ na ukiingia huufikii mlango wa nyumba kwani kuna ‘kamwendo’.
Nje ya nyumba hiyo kuna ‘parking’ ya magari madogo zaidi ya kumi huku chini kukiwa na tarazo na pembeni kuna bustani nzuri iliyopandwa maua ya kuvutia.“Amehamia hivi karibuni, anaonekana muda wa kutoka na kuingia tu.
Nyumba anayoishi staa huyo.
“Lulu ni binti mrembo mwenye mvuto wake, ukizingatia ana nyota pia ya kupendwa, kwa hiyo siyo mtu wa kukaa uswazi,” alidai mtoa habari wetu na kuongeza:
“Bidada kaula maana nasikia jamaa ameahidi kumpa matunzo ya nguvu. “Alianza kwa kumnunulia lile gari la kifahari la Toyota Rav4 New Model analotembelea Lulu, sasa naona kamuweka pazuri na kweli nyumba inaendana na hadhi yake.
ADAIWA KUMPA JEURI YA KUWAFUNIKA KAJALA, WEMA “Nasikia jamaa amempa jeuri ya kuwafunika kabisa Kajala (Masanja) na Wema (Sepetu) ambao inasemekana wana mkwanja wa kumwagamwaga ovyo.”
LULU LAIVU! Kupitia Kipindi cha Nirvana kinachorushwa na EATV, Lulu alionekana ndani ya mjengo huo uliojaa mazagazaga ya thamani.Mjengo huo una makabati makubwa ya nguo na viatu kiasi kwamba mtu unaweza ukahisi umeingia kwenye duka la nguo (boutique) na viatu kibao.
Akizungumza kwa kujiamini Lulu alisema kuwa anapenda vitu vizuri hasa linapokuja suala la kupiga pamba ndiyo maana amejaza pamba kali kwenye makabati.“Kimsingi sipendi shida, napenda kuvaa vizuri, kula vizuri, kulala pazuri na mambo yote mazurimazuri,” alisema Lulu.
Elizabeth Michael ‘Lulu’,akiwa kwenye pozi.
BILIONEA GANI? Ili kupata undani wa mwanaume huyo, gazeti hili lilichimba ambapo kwa mujibu watu wa karibu na Lulu, jamaa huyo ni mfanyabishara mkubwa wa madini jijini Arusha.
“Kama mtakumbuka, huyo jamaa aliwahi kuwagombanisha Lulu na Husna (Maulid) kwani mwanzoni alikuwa mwanaume wa Husna.“Hivi unajua kabla ya ishu hiyo, Lulu na Husna walikuwa mashosti lakini baadaye wakawa kama paka na panya kisa tu ni huyo bilionea,” kilidai chanzo hicho.
LULU ASAKWA

Baada ya kunyetishiwa habari hiyo ya mtaani, gazeti hili lilimsaka Lulu hadi nyumbani kwake na lilipomkosa lilimtafuta kwa njia ya simu na alipopatikana alifunguka:
“Kiukweli kabisa nyumba ninayoishi sasa mimi na familia yangu siyo kwamba nimepangishiwa wala kununuliwa na sijui bilionea au kigogo yeyote, hayo ni maneno ya watu tu. Unajua watu wanaongea sana, wanadhani mimi siwezi kujimudu,” alisema Lulu kwa kujiamini.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname