SI LAZIMA NIJUE KIINGEREZA
Mkurugenzi wa Kampuni ya filamu Rj Company,Vicenti Kigosi amesema si
lazima kujua Kingereza maana hata Messi hajui, Ray amesema hayo
alipokuwa akichat Live na mashabiki zake kupitia ukurasa wa Facebook wa
EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachokukutanisha na watu
mahiri kila siku ya jumatano kuanzia saa sita za mchana mpaka nane
kamili. Mkali huyo ambae kwa sasa anachukuliwa kama
moja ya watu wenye mafanikio katika tasnia ya filamu nchini ambae pia
ameshawishi vijana kibao kuingia katika tasnia hiyo amefunguka na kuweka
wazi kuwa suala la lugha ya kiingereza kwake ni changamoto lakini si
jambo la ajabu sabgabu kuna watu wengi maarufu duniani wanapigwa chenga
na lugha ya kiingereza.
Prince Dully >>>>Mbona haujui kingereza au uliishia darasa la saba,nini?
RAY Kigosi >>>>>>Hata messi hajui kiingereza kwani mimi muingereza nijue Kiingereza.
No comments:
Post a Comment