Mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Habash ‘G. Habash’ akiwa na Miss Mara 2000, Rashida Wanjara.
Gardner
Gabriel Habash ‘G. Habash’ na ‘mtalaka’ wake, Judith Wambura Mbibo
‘Jide’, Jumamosi iliyopita walifanya tukio lililowashangaza watu
kufuatia kila mmoja kuingia ukumbini akiwa na kampani yake na kukwepana kama paka na panya, Amani liliwanasa kwa vile lilikuwepo.Tukio
hilo lililoamsha minong’ono kwa watu waliosoma mchezo mzima, liliibukia
ndani ya Ukumbi wa Ten Lounge (zamani Business Park) uliopo Makumbusho,
Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambako kulikuwa na uzinduzi wa albamu
ya Bongo Fleva.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Gardner alipoingia alikwenda kukaa
kwenye meza na watu wengine watatu, baadaye akafika Miss Mara 2000, Rashida Wanjara na kuunga ambapo walikuwa wakibadilishana mawazo na kufunguliana vinywaji kwa meno na kumiminiana kwenye glasi.
kwenye meza na watu wengine watatu, baadaye akafika Miss Mara 2000, Rashida Wanjara na kuunga ambapo walikuwa wakibadilishana mawazo na kufunguliana vinywaji kwa meno na kumiminiana kwenye glasi.
JIDE NAYE
Wakati Gardner ambaye
pia hujulikana kwa jina la utani la Kapteni akiendelea kujipoza na
Rashida na wengine, Jide yeye alikaa meza moja na kijana mmoja
aliyevalia shati la kitenge la mtindo uliowahi kutamba miaka mitano
nyuma, wengine huita Mackezie sanjari na wadada wawili.
WALICHOTAKA WATU
Baadhi
ya watu walisikika wakishauri kwa sauti ushauri ambao haukuwafikia
wawili hao ambapo walisema kama kweli ndoa hiyo haijavunjika, ni vyema
Jide angeenda kwenye meza aliyokaa Gardner na kusema chochote kisha
kuondoka hali ambayo hakuwepo.
‘Mtalaka’ wa Gardner, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ (kulia) akijaribu kukwepa kamera za Global.
PAKA NA PANYA!
Mtu
mmoja aliyekuwa amehudhuria shughuli hiyo na mkewe, alimuita paparazi
wetu na kumuuliza: “Kwani, Jide na Gardner sasa ni paka na panya?”
Mwandishi: “Kivipi?”
Mtu: “Namwona Jide
yuko na kampani yake, Gardner naye na kampani yake kule. Unajua paka na
panya ni vigumu kukutana! Hawa kweli hawapo sawasawa,” alisema mtu huyo
alijitambulisha kwa jina la Yahya.
Akaendelea: “Unajua
ninavyojua mimi, Gardner ni kijana mpole sana, mwenye upendo, ila Jide
ni mkali. Halafu kwa sababu yeye Jide ana pesa naamini alitaka kumpandia
kichwani mumewe wakati anajua yeye ni kichwa cha nyumba. Pesa na ndoa
mambo mawili tofauti.”
WAWINDWA NA KAMERA
Muda mwingi paparazi
wetu aliwavizia Gardner na Rashida na kufanikiwa kuwafotoa picha kadhaa
lakini kimbembe kilikuwa kwa Jide ambaye alionekana kuwa makini na
kukwepa kamera ya paparazi wetu mara kadhaa huku akionekana kuwa na hasira na kuna muda meza yake iliparaganyika baada ya mwanga wa kamera kuwamulika yeye na kampani yake.
ANGALIA HII
Katika
hali iliyodhihirisha wawili hao hawako sawasawa, muda f’lani Gardner
aliinuka na kuelekea upande aliokaa Jide ambapo mwanamuziki huyo naye
alionekana kama kutaka kukimbia na kumfanya Gardner kubadili mwelekeo wa
safari yake.
Gardner akiendelea kufatilia jambo.
KUNA HII PIA
Mmoja
wa mashuhuda aliyekuwa ukumbini hapo naye alimwambia paparazi wetu
kuwa, aliwaona wawili hao wakikwepana baada ya kukutana kwenye njia ya
kuelekea maliwatoni.
GARDNER AZUNGUMZA NA AMANI
Juzi, Amani
lilimtafuta Gardner kwa njia ya simu na kumuuliza ni kwanini yeye na
Jide kila mmoja aliingia ukumbini na kampani yake.Gardner: “Kaka, yeye
(Jide) alikwenda pale kumpa tafu yule aliyekuwa akizindua albamu yake
pale. Sasa isingekuwa rahisi tugandane pamoja kila wakati. Lakini hayo
unayoniambia ni madai tu.”
TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni, ndoa ya wawili hao iliripotiwa kuvunjika na kila mmoja kushika njia yake huku Gardner
akiwa anakanusha mara kwa mara kwamba ndoa ipo imara. Jide naye amekuwa
akiweka kwenye mtandao wa Instagram picha yake yenye kidole cha pete ya
ndoa bila maelezo!! Ni shiida!
No comments:
Post a Comment